Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Sikonge

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Rais Samia Suluhu Hassan amepeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Shaka ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo waliofika kumsikiliza alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Sikonge ambayo ujenzi wake umegharimu Sh.bilioni mbili zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Na ndio maana ametutuma tuje tufanye kazi kwanza ya kukagua maendeleo , ameamua kuleta fedha nyingi ndani ya mkoa huu wa Tabora na ambazo anazileta ndani ya Wilaya ya sikonge

“Vile vile tumekuja kukagua uhai wa chama chetu na utekelezaji wa Ilani ya chama chetu ambacho ndicho kimeunda Serikali, nichukue fursa hii kumpongeza Rais Samia kwa fedha nyingi za maendeleo alizozileta katika wilayani hapa.

“Sasa fedha nyingi zilizoletwa ziandane na kasi za utekelezaji wa maendeleo endelevu ambayo Rais ameelekeza yafanyike kupitia miradi ya kimkakati ndani ya Wilaya hii ya Sikonge, bahati nzuri Rais anajua na anafahamu mahitaji ya wanachi anawaongoza

“Kwa hiyo kila Wilaya na kila mkoa Rais ametoa vipaumbele na cha kwanza ni huduma za afya kwa jamii na ndio maana tunaambiwa hapa Sikonge kwenye Hospitali hii ya Wilaya ameleta Sh.bilioni mbili. Sasa ujenzi huu wa miradi hii mikubwa ya maendeleo uandane na utoaji bora wa huduma kwa wananchi,”amesema Shaka.

Ameongeza katika historia ya nchi hii Rais Samia amekuwa wa kipekee kwani huko nyuma ilizoeleka majengo yanajengwa baadae yanabaki kuwa mazalia ya ndege lakini sasa wanajenga na vifaa tiba vinaletwa kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.

Niwaombe wauguzi, madaktari pamoja na wote ambao mnahusika kwa njia moja ama nyingine katika kutoa huduma hizi kwa wananchi lazima muwe rafiki kwa wateja wenu.

“Lazima mtengeneze mazingira bora ya kuhakikisha huduma hizi ziendane na kasi ambayo Rais wetu amekuwa akiionesha bahati mbaya sana na kwa masikitiko makubwa na hili naomba niseme kwa wilaya hii ya sikonge kwenye miradi hii ya maendeleo kasi ya ukamilishaji miradi sio nzuri sana katika Wilaya hii.”

Ameongeza haifurahishi fedha zinakuja lakini kasi ya ukamilishwaji wa miradi na uanzishwaji wa miradi imekuwa ikisuasusa jambo hilo sio nzuri , spidi yao imekuwa ndogo na kwamba panapotokea pakalegalega CCM haiwezi kufunga funga maneno na hawawezi kukaa kimya.


Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka Akizungumza na Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora kwa Njia ya Simu wakati akitatua Changamoto ya Ukosefu wa Huduma ya Maji kwa wananchi wa kata ya Tumbi.



Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, akisoma moja ya mabango ya Wananchi waliofika katika ziara ya ukaguzi wa Kiwanda Nyuzi Mkoani Tabora


Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Akifurahi wakati akizungumza na Wananchi, katika ziara ya ukaguzi wa Kiwanda Nyuzi Mkoani Tabora.
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akitazama mitambo katika kiwanda cha kuchakata asali wilayani Sikonge, Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani humo. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Sikonge waliohudhuria mkutano wakati wa Ukaguzi wa maendeleo ya Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...