Njombe
WANANCHI wa kijiji cha Amani kilichopo kata ya Mundindi halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wameeleza kusikitika kutokana na kuvamiwa na jamiii inayotajwa kuwa ni ya kabila la Mang’ati huku wakipigwa viboko,kupokonywa silaha pamoja na Ng’ombe 27 ndani ya kijiji chao.

Wananchi wa kijiji hicho wametoa kilio chao katika mkutano wa mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga huku wakibainisha kuwa kitendo kilichofanywa na jamii hiyo kutoka mkoa jirani wa Ruvuma kimeanza kusababisha chuki baina yao na Wapangwa.

“Kwanza kuna matukio mawili la kuibiwa Ng’ombe 27 na kupigwa viboko na wenzetu wa kabila la Mang’ati waliokaribishwa maeneo ya Madaba,sis hatuwakatai wenzetu lakini hili wanalofanya kwa kweli hali imekuwa mbaya na wamenyang’anya na bunduki ya mtu”Amesema Thadei Luoga mkulima na mfugaji ambaye ni muhanga wa kijiji hicho

Mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga amesema kijiji hicho ni cha Amani na anataka amani itawale huku akiahidi kushirikiana na wanakijiji mpaka haki yao itakapopatikana huku polisi msaidizi wa kata hiyo A/INSP Asifiwe Mwampashi akibainisha kuwa tayari jambo hilo lipo mikononi mwa polisi na limekwishaanza kufanyiwa kazi na vyombo via usalama.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...