VICTOR MASANGU, PWANI
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanya uchunguzi na kukagua miradi 32 ya maendeleo yenye thamani ya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni Saba na kubaini miradi nane kuwa na kasoro na mapungufu mbali mbali ambazo zimesababishwa na kamati kutowajibika ipasavyo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Christopher Myava wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa majukumu katika robo ya tatu ambapo amesema kuwa baadhi ya miradi umechelewa kutokana na uzembe wa wahusika kutofanya kazi kwa kuchelew.

Aidha Mkuu huyo alibainisha kuwa katika miradi mingine Kuna tabia ya baadhi ya mafundi kujichukulia vifaa vya ujenzi bila ya kukabidhiwana wanakamati hali ambayo inapelekea upotevu wa vifaa vya ujenzi hivyo kuathiri suala zima la ubora wautekelezaji wa miradi hiyo.

"Katika uchunguzi wetu ambao tumefanya Takukuru tumeweza kubaini miradi nani ya maendeleo kuwepo kwa mapungufu na kasoro mbali mbali ambapo kwa sasa tunaendelea na uchunguzi zaidi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wale wote ambao watabainika kuhusika na vitendo vya rushwa.

Pia alisema kuwa katika kukabiliana na winbi la mianya ya rushwa wataendelea kuweka mipango madhubuti kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma na kufanya uchunguzi wa Mara kwa Mara katika sekta mbali mbali lengo ikiwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa.

"Ili kuweza kudhibiti mianya ya rushwa katika idara za serikali pamoja na sekta binafsi jumla ya chambuzi za mifumo ipatayo Saba zimefanyika kwenye sekta za elimu.huduma za jamii,madini.mapato,kilimo ,ardhi pamoja na maji,"alisema Christopher.

Alifafanua zaidi aliongeza kuwa pia wamegundua kuwepo kwa ukwepaji wa kulipa ushuru katika eneo la madini ya ujenzi ambapo wamebaini kwamba maeneo mengi ya uchimbaji wa madini hasa ya mchanga hakuna udhibiti wa kutosha.

Aidha Mkuu huyo wa Takukuru amesema kuwa pia wamebaini kuwepo kwa maduka ya dawa muhimu kuendesha shughuli zao kinyemela bila ya kuwa na leseni kitu ambacho ni kinyume kabisa na Sheria na taratibu za nchi.

Pia katika hatua nyingine ametoa onyo Kali kwa baadhi ya watu ambao ni wabadhilifu katika mali za umma na kuwahimiza wananchi wa Mkoa wa Pwani kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.
Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Mkoa wa Pwani Christopher Myava akizingumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na utekelezaji wa robo ya tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...