Na Pamela Mollel,Arusha

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa limejipanga kuongeza idadi ya watalii wa ndani kwa kutoa elimu ya utalii pamoja na kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi zetu kupitia maonyesho ya nane nane

Pia shirika hilo ni miongoni mwa washiriki walioshiriki katika sherehe za nane nane kanda ya kaskazini katika viwanja vya Themi jijini Arusha

Akizungumza na vyombo vya habari katika banda lao la maonesho Afisa uhifadhi daraja la kwanza Jerome Boniface alisema kuwa lengo la kushiriki maonyesho hayo ni kuunga mkono jitihada za Rais kutangaza vivutio na kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania

"Tumeona matokeo makubwa ya Royal tour sasahivi tuna wageni wengi kutoka nje ya nchi wanaokuja kutembelea vivutio vyetu lakini utalii wa ndani bado idadi ni ndogo"alisema Jerome

Alisema kwa asilimia kubwa wanaokuja katika maonyesho hayo ni wakulima,wajasiriamali wafanyabiashra na watu wengine ambao watapata fursa ya kujua umuhimu wa utalii wa ndani

"Tumebarikiwa sana na Mungu kuwa na vivutio vingi tunawaomba wananchi kutembea vivutio hivyo na gharama yake ni nafuu sanaaa"alisema Jerome

Aidha alisema kuwa wapo bega kwa bega na Rais Samia Suluhu Hassan hivyo watu wajitokeze katika zoezi la sensa litakalo fanyika August 23 mwaka huu.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...