*Ni kuhatarisha usalama wa mifugo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa wito kwa wafanyabiashara wanauza Dawa za Mifugo kuacha kuuza Dawa katika magulio na badala yake kufuata utaratibu uliokweka kisheria wa kuwa na maduka maalum ya Dawa hizo.

Akizungungmza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya, Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mshigati amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanauza Dawa za mifugo kwenye maeneo ya wazi yakiwemo magulio jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

"Moja ya jukumu letu ni kusimamia Dawa za Mifugo zisiuzwe kiholela kwa kuhakikisha Dawa hizo zinahifadhiwa vizuri kwenye maduka maalum na yamesajiliwa"Amesema Meneja TMDA Kanda za Nyanda za Juu Kusini.

"Uuzaji wa Dawa za Mifugo kiholela una madhara kwa wanyama na kwenda kwa binadamu kutokana na kukosa maelekezo sahihi namna ya kuzitumia.

Amesema TMDA imeshiriki kwenye Maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali wa kilimo na mifugo juu ya majukumu yake katika sekta ya dawa na Vifaa Tiba na kwamba moja ya jukumu lake ni kusimamia Dawa hizo na kuhakikisha wale wote wanaofanya bishara ya kuziuza wanafuata taratibu zilizowekwa.

Mshigati ametoa wito kwa wananchi kununua Dawa hizo kwenye maduka maalimu yaliyosajiliwa kisheria ambayo ndiyo yanakuwa na wataalam wa dawa hizo sambamba na kufuata maelekezo ya wataalamu hao ili kuepuka kuleta madhara kwa mifugo na kukosa msaada wa kitaalamu pindi wanapotatizo.
Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mshighati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo wakati akielezea kuhusu udhibiti wa dawa za mifugo katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Anitha Mshighati akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la mamlaka hiyo wakati katika Maonesho ya Kilimo-Nane Nane 2022 yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya.
Afisa Elimu kwa Umma TMDA Mariam Sanga  (kushoto) na  Jofrey Kikoti (kulia) Mkaguzi wa Dawa Msaidizi wa TMDA wakimsikiliza mmoja wa wananchi waliopita katika banda hilo na  kuuliza swali na kuweza kupata majibu.
Afisa Elimu kwa Umma TMDA  Mariam Sanga kushoto) akimhudumia mwananchi aliyetembelea  banda lao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...