Wakazi wa Jimbo la Kasulu mjini wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kutekeleza kwa kasi miradi ya Maji, Barabara na Afya katika jimbo hilo lenye kata 15, ambapo kukamilika kwa miradi hiyo kutatatua kero zao za muda mrefu.

Wakazi hao wamebainisha kuwa katika jimbo la Kasulu mjini katika sekta ya Afya, ujenzi wa vituo vya Afya viwili, Zahanati tano, Wodi ya wazazi na Jengo la wagonjwa mahtuti upo katika hatua ya kukamilika. Aidha, tayari barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa Kilometa 260 zitajengwa kuiunganisha jimbo hilo na maeneo mengine.

Wakiongea wakati wa Mkutano wa Mhe. Joyce Ndalichako ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo na pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wamemshukuru Mbunge huyo kwa kufikikisha kero zao kwa Mhe. Rais na kuzipatia ufumbuzi ambapo tayari miradi ya maji utekelezaji wake wa upanuzi wa Mtandao wa mabomba na shughuli za uchumbaji visima unaendelea.

Mhe. Ndalichako amewahakikishia wanakasulu mjini kuwa ataendelea kuzishughulikia kero za muda mrefu kwa kusogezwa karibu huduma muhimu za kijamii kwa wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maemdeleo.

Aidha, Mhe. Ndalichako amefafanua kuwa Mhe. Rais Samia katika jimbo hilo katika jimbo tayari amewawezesha ujenzi wa shule mpya mbili, vyumba vya madarasa 57, ukamilishaji wa maboma 15 na ujenzi wa nyumba za walimu mbili. Mbunge huyo amefanya mikutano katika maeneo ya Ruhita, Kanazi ,Msambala na Kabanga ambapo ameweza kuwaeleza wananchi juu ya shughulii zinazotekelezwa na serikali katika jimbo hio, Aidha, amewahamasisha kushiriki katika zoezi Sensa ya Watu na Makazi itakayo fanyika tarehe 23 Agosti, 2022.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...