Na Janeth Raphael - Kigoma
SERIKALI wilayani Kakonko Mkoani Kigoma imewataka wananchi kutowanyanyapaa watu wenye ulemavu badala yake kuwajali,kuwahudumie na kuwapa mahitaji yote ya kibinadamu.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Evance Mallasa,Wakati akishuhudia makabidhiano ya baiskeli saba za walemavu zilizokabidhiwa na Mbunge wa jimbo la Buyungu,Aloyce Kamamba,kwa walengwa kata mbalimbali.

Mallasa amesisitiza jamii kuendeleza kuwathamini walemavu hao kwa madai kuwa ulemavu siyo ugonjwa na kwamba hayo ni maumbile ambayo Mwenyezi Mungu ilimpendeza kufanya hivyo.

Akikabidhi msaada huo,Mbunge Kamamba,amedai analazimika kuzitumia fursa zote za maendeleo ambazo zinamanufaa kwa wananchi wa jimbo lake kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na fursa hizo.

Aidha amewasisitiza kuzitunza baiskeli hizo Ili ziweze kuwasaidia kurahisisha shughuli zao Kwa kujitafutia kipato na kuinua uchumi wao.

Kwa upande wake kaimu Ofisa ustawi wa jamii Wilaya ya Kakonko, Hellen Hurdson,mbali na kumpongeza Mbunge huyo ameomba msaada kama huo uendelee kutolewa kutokana na Wilaya hiyo kuwa na walemavu zaidi ya 1790.

Akiongea kwa niaba ya wenzake,Neema Bakari,ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Kasungwa emeshukuru Kwa msaada huo na kwamba baiskeli hiyo itamsaidia kufika shuleni Kwa wakati.

Msaada wa baiskeli hizo unatarajiwa kuwa endelevu baada ya wahisani shirika lisilo la kiserikali la "Peace for Conservation" la jijini mwanza kuahidi kumfadhili Mbunge huyo baiskeli zingine 13 ambazo kila moja itagharimu kiasi cha shilingi 500,000 Ili kuunga mkono juhudi zake za maendeleo kwa jamii.
Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma Kanali Evance Mallasa, anayefuata ni Mbunge wa Buyungu Aloyce Kamamba aliyefunga mikono pamoja n a Mkurugenzi WA "Peace for Conservation Daudi Kabambu wakiwa pamoja na baadhi ya watendaji wa ofisi ya CCM Wilayani Kakonko Mkoani kigoma na badhi ya watu wenye ulemavu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...