Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe


Zaidi ya watu 300 wilayani Kisarawe mkoani Pwani ,waliokuwa hawajui kusoma ,kuandika na kuhesababu akiwemo kikongwe Ramadhani Rashid mwenye miaka zaidi ya 80 wamejitokeza kupatiwa elimu ya watu wazima.

Elimu hiyo ni mpango wa Serikali MEMKWA na MUKAJA ikiwa njia moja wapo ya kupunguza idadi ya watu wenye changamoto ya kutokujuwa kusoma na kuhesabu ambapo inakadiriwa kufikia watu 3,000 wilayani humo hawajapata fursa ya kujua kusoma .

Kivutio kikubwa ni kwa mzee Rashid ambae ni kikongwe aliyejitokeza kupata mafunzo hayo, katika shule ya msingi Gwata ili kujikwamua na changamoto ya kutokujua kusoma kuandika na kuhesabu .

Mzee Rashid alisema ,hakufanikiwa kujua kusoma wala kuandika kutokana na Mazingira yaliyokuwepo kwenye maisha yake huko nyuma ,hivyo baada ya kusikia mpango huo ,amejiunga na mpango huu ili kuondokana na usumbufu aliokua akiupata pindi alipokuwa akiuza kitu, anapotumiwa jumbe za maandishi katika simu yake ya mkononi na kushindwa kuwa na usiri kwani alikuwa anasomewa message zake.

Alisema pia tatizo kubwa lilikuwa zaidi pale linapokuja suala la mikataba ya mauziano ya mashamba ama viwanja.

Mnufaika mwengine wa elimu ya watu wazima ni Saidi Chakupata na Mwazani Rajabu ambao waliishukuru Serikali kwa kuanzisha suala hilo muhimu na Sasa wanaweza kusoma na hata kuandika .

Ofisa elimu awali na msingi Kisarawe ,Khadija Mwinuka alieleza, mkakati wa Serikali wa kupunguza idadi ya wasiojua kusoma kuandika na kuhesabu kupitia MEMKWA na MUKAJA program zinaendeshwa kote nchini.

Alieleza, anaamini wanaopata mafunzo hayo kupitia MEMKWA wanakwenda kuwa mabalozi wa kumzungumzia umuhimu wa mpango huo.

Khadija alisema kwamba, wengine wanakuwa wanaona aibu kujitokeza ,wasione aibu kwani elimu haina mwisho.

Ofisa elimu watu wazima , Esther Senkoro alifafanua, baadhi ya watu wazima wasiojua kusoma kwasasa wamekuwa na mwamko baada ya kuona wenzao kukwiva kupitia mpango huo .





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...