KAMPUNI ya meridianbet imeongoza zoezi la usafi katika maeneo ya bustani inayomilikiwa na serikali Upanga, Mtaa wa Charambe. Serikali ya mtaa wa Charambe pia ilishiriki zoezi hili.

Kampuni hii imeshirikisha wadau mbalimbali wanaozunguka eneo hilo, wakiwemo wafanyakazi na wafanyabiashara wa maeneo hayo. Serikali ya mtaa, ikiwakilishwa na mwenyekiti na mtendaji nao walishiriki kuunga mkono jitihada za kampuni ya Meridianbet.

Afisa masoko wa kampuni hii, Twaha Mohammed akiwakilisha kampuni ya Meridianbet amesema wanafurahi kushirikiana na serikali na majirani kufanya usafi wa mazingira kama muendelezo wa wajibu wao kwa jamii.

"Nimefurahi sana, ikiwa ni mwendelezo wa ushiriki wetu kwenye masuala ya kijamii. Wki iliyopita tulitoa vifaa vya usafi na vifaa tiba kwenye hospitali ya Madale, kwa kumalizia mwezi huu tukaona tufanye usafi hapa Upanga, tushirikiane na wananchi na serikali" – Afisa Masoko, Meridianbet

Kwa upande wa mwenyekiti, wa serikali ya Mtaa mwenyekiti amesema amefurahi sana kushiriki zoezi hili, na angependa eneo hili lishughulikiwe kila mwezi kwa ushirikiano wa majirani wote wa eneo hilo.

“Eneo hili ni vyema tushirikiane, ili tufanye usafi kwa pamoja kila mwezi. Alitoa wito kwa wafanya biashara wa eneo hilo kuzingatia usafi na kuhakikisha mazingira yako salama”

Meridianbet wamekuwa na utaratibu wa kushiriki shughuli za kijamii, na kurejesha kwa Jamii. Wakishiriki shughuli za kimichezo, misaada kwa makundi maalumu na udhamini.

Meridianbet ni Kampuni bora na kongwe ya ubashiri Tanzania, ambayo imejipambanua kwa kutoa ofa bora za ubashiri wa michezo mingi, wakiwa na zaidi ya michezo 6000 ya kasino ya Meridianbet. Meridianbet pia hushirikiana na waandaaji wa michezo ya kasino kuendesha Jackpot za michezo ya kasino.

Jisajili na ubashiri na meridianbet kupitia www.meridianbet.co.tz, au piga *149*10# kubashiri bila intaneti ukiwa na mtandao wa Tigo na Airtel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...