*Dawa hiyo imesaidia kuimarisha afya watimiaji wa dawa za kulevya na kutotamani kutumia dawa hizo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MTAFITI na mtaalam wa tiba asili, Khalid Hussein Bwenya amegundua dawa ya asili ya kumsaidia mtu ambaye ameathirika na dawa za kulevya na kumuondoa katika utegemezi wa dawa hizo.

Dawa hiyo inamfanya mtumiaji wa dawa za kulevya asili kuchukua nafasi ya dawa nyingine za kisasa ambazo malengo yake ni kuiondoa jamii katika madhara hao ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinarudisha nyuma maendeleo ya vijana.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kigamboni jijini Dar es Salaam Dk Khalid Bwenya aliweka bayana malengo ya mtafiti huo kuwa utasaidia serikali kupunguza gharama kubwa za kukabili tatizo la watumiaji wa dawa dawa za kulevya 'mateja'.

Amesema watumiaji wa dawa za kulevya 'mateja' ni janga kwa taifa na Dunia kutokana na vijana wengi kutokuwa na mchango kwa ujenzi wa Taifa badala yake kuwa mzigo pamoja na kero kwa familia yake.

Watumiaji dawa za kulevya wamekuwa tabia ambazo hizikubaliki katika familia zao na jamii kwa ujumla kutokana na kuwa sehemu ya wahalifu wa wizi.

Dk Bwenya amekuja na jawabu la kukabili uteja kupitia dawa ya asili ambayo ndani ya siku 15, mraibu anarejea katika hali yake kama ilivyokuwa kabla ya kutumia mihadarati.

Dk Bwenya mtaalam na mtafiti wa tiba za asili anasema dawa hiyo ni suluhisho la tatizo la uteja, ugunduzi uliopata suluhu yake tangu mwaka jana.

Amesema dawa hiyo inatokana na mchanganyiko wa matunda mbalimbali na mitishamba ipo katika mfumo wa kimiminika ambako mbali na kutibu tatizo la uteja pia linatoa sumu mwilini, inaondosha gesi tumboni, kutoa sumu kwenye ubongo.

Aidha amesema Kuhusu ufanisi wa dawa hiyo ni utafiti aliyoifanyia kwa zaidi ya miaka 20 kubaini ina uwezo mkubwa wa kukabili tatizo la uteja kwa siku 15.

Anasema muda huo wa siku 15 unatosha kuleta matokeo chanya iwapo muathirika atatumia dawa hiyo kama alivyoelekezwa.

"Kama muathirika wa dawa za kulevya (Haijalishi ametumia dawa za kulevya kwa miaka mingapi) atazingatia maelekezo ya utumiaji wa ndani ya siku 15, matokeo yataanza kuonekana," alisema Dk Bwenya.

Amesema uchunguzi wao umebaini kwamba dawa hiyo ya ikitumika ipasavyo ina matokeo mazuri na kwa haraka ukilinganisha na dawa za kisasa.

Kuhusu athari za utumiaji wa dawa zake.
Amesema tofauti na dawa za kisasa ambazo husababisha mning'inio (hangover) kwa mtumiaji kwa upande wa dawa zake haisababishi hali hiyo.

Aidha ili kufanikisha matarajio yake ya kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya, anajipanga kuwa na shamba la ekari 500 kwa ajili ya kupanda miti ya aina mbalimbali ambayo ni tiba ya maradhi mengi ambako pia ataweka kiwanda kikubwa kwa ajili ya uzalishaji wa dawa.

Alisema utafiti wake ameufanya kwa kusoma vitabu mbalimbali, majarida sambamba na kuongea wataalam wengi na kufanikiwa kutengeneza dawa hiyo ambayo ni mkombozi kwa vijana wa kitanzania.

Dk Bwenya alisema utafiti wake wa kwanza alianzia Afrika Kusini mwaka 2001 katika jiji la Cape town ambako amejifunza mambo mengi ambayo yalifungua njia ya kufikia suluhisho la upatikanaji wa dawa ambayo ni mkombozi kwa vijana na jamii kwa ujumla.

"Kwa sababu kazi nnayofanya ni kwa ajili ya jamii ya watanzania na waafrika wote, naiomba serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi waniunge mkono kwani jambo ninalofanya linatuhusu sote, nawaomba wanishike mkono katika hili," alisema Bwenya.

Naye mzazi wa Juma Selemani Saleh ambaye ni muathirika wa dawa za kulevya alisema mtoto wake huyo alikuwa tegemezi lake ambako alitumia dawa za hospitali kwa zaidi ya miaka sita lakini hakupata nafuu ila hivi karibuni alipokutana na Khalid akampatia dawa na hivi sasa mtoto wake anaanza kupata nafuu.

Saleh alisema mtoto wake huyo kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya aliwahi pia kufanyiwa operesheni ya utumbo.

"Nilikutana na Dk Khalid Kigamboni akitafuta nyumba kwa ajili ya kupanga ili aweke kituo chake, ndipo alipopata nafasi ya kukutana naye.

Naye Juma Selemani alisema baada ya kutumia dawa ya Dk Khalid kwa siku ya kwanza aliharisha na kutapika lakini baadaye alianza kupata hamu ya kula, akaanza kupiga chafya na mwili kuanza kupata nguvu.

Aliwaasa vijana wenzake kuachana na matumizi ya dawa za kulevya kwani wao ni nguvu kazi inayotegemewa na Taifa.

Selemani alisema kwa vijana wenzake waliochoka kuvuta unga na kujutia nafsi zao, wajitokeze kupata dawa bila gharama yoyote.
Mtafiti wa Dawa za Asili Dk.Khalid Bwenya akimpatia dawa Juma Seleman kwa ajili ya kutoa sumu ya Dawa za Kulevya wakati alipomtembelea kwa mara nyingine baada ya kuimarika kwa afya yake kutokana na kutumia dawa hiyo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mtafiti wa Dawa za Asili Dk.Khalid Bwenya akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomtembelea Juma Seleman muathirika wa dawa za kulevya kwa kumpatia dawa ya asili kwa ajili ya kutoa sumu ya Dawa za Kulevya ambapo afya ya Juma imeanza kuimarika kutokana na kutumia dawa hiyo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...