Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewataka watendaji wa serikali kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya TASAF nchini, ukiwemo wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Budekwa wilayani Maswa ili kuunga mkono jitihada ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuliletea taifa maendeleo.

Ndejembi ametoa wito huo, mara baada ya kukagua ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Budekwa akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kijiji cha Kiloleli wilayani Maswa.

Naibu Waziri Ndejembi amesema, njia pekee ya watendaji wa serikali kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya TASAF ni kuwahamasisha wananchi kushiriki utekelezaji wake kuanzia ngazi ya kijiji, kata, tarafa hadi wilaya ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

Ndejembi ameongeza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa kupeleka mradi huo wa ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Budekwa ili kuwalinda na kuwaepusha watoto wa kike na changamoto zinazokwamisha malengo yao katika elimu.

“Mwanafunzi anapoishi katika mazingira ya shule kutokana na uwepo wa bweni, itamsaidia fikra zake zote kuzielekeza katika masomo, na hilo ndio lengo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan,” Amesema Ndejembi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...