Serikali imewahakikishia wadau wa Uchukuzi nchini kuwa itaendelea kufanyia kazi na kuchukua hatua za haraka changamoto mbalimbali zinazowasilishwa na wasafirishaji nchini na nchi jirani lengo likiwa ni kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, na wadau wa usafirishaji katika kikao cha 16  Katibu Mkuu wa  Uchukuzi Gabriel Migire, amesema nchi Jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Zambia, na Malawi zimekuwa zikisafirisha mizigo mbalimbali kupitia bandari ya Dar es Salaam hivyo  Serikali inafanya kila inaloweza  kuhakikisha biashara inafanyika bila vikwazo.

“Tunashukuru kwenye suala la biashara ngazi zote za Serikali zimekuwa zikilitazama jambo hili kuanzia uongozi wa juu kwa ushirikiano mzuri sana lengo ni kuhakikisha kuwa malengo yote yaliyopangwa katika urahisishaji wa uingiaji na utoaji wa mizigo unazingatiwa” amesisitiza Katibu Mkuu Migire.

Katibu Mkuu Migire amesema miongoni mwa matokeo chanya ya vikao vya mara kwa mara vya kusikiliza changamoto za wadau wa usafirishaji ni pamoja na kuongezeka kwa mchango wa bandari katika pato la Serikali ambapo limefikia  asilimia 41 kutoka asilimia 38 kwa miezi michache iliyopita..

Aidha, Katibu Mkuu Migire  amesisitiza umuhimu wa taasisi zilizopewa jukumu la kuunganisha mifumo ya TEHAMA kuharakisha zoezi hilo ili kupunguza adha kwa wasafirishaji wanaolazimika kupitia taasisi mbalimbali ili kupata vibali vya kuchukua mizigo yao inapowasili.

Naye Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Mrisho Mrisho amesema kwa sasa  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inafanyia kazi suala la kupunguza muda wa meli kupakia mizigo ili kuweza kuhudumia meli nyingi zaidi kwa wakati mmoja

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Tanzania (ITDA) Adam Mwenda ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwakutanisha wadau wa usafirishaji na kusikiliza changamoto mbalimbali walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja na kwa wakati.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire, akisisitiza jambo katika Kikao cha 16 cha Wadau wa Usafirishaji (hawapo pichani), wakati alipokutana nao jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Tanzania (ITDA), Adam Mwenda, akionesha mapendekezo ya vibao vinavyopendekezwa kutumika kwa magari yanayokwenda nje ya nchi kutokea Bandari ya Dar es Salaam kwa Wajumbe wa Kikao cha 16 cha Wadau wa Usafirishaji (hawapo pichani), kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wadau wa usafirishaji wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire (hawapo pichani), katika Kikao cha 16 cha wadau hao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

PICHA NA WUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...