Na Mwandishi wetu, Longido

Taasisi ya Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa jamii (CORDS) jana imekabidhi darasa lililojengwa maalum kwa Vijana wa jamii ya Kimasai wa kike na kiume ,ambao wamekosa fursa ya kusoma katika mfumo rasmi shule ya Msingi (MEMKWA).

Darasa hilo limegharimu kiasi cha sh 33.5 milioni lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 45 na litakuwa katika shule ya msingi Ngoswak iliyopo kata ya Engareinabor wilaya ya Longido mkoani Arusha na limejengwa na shirika hilo la CORDS.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa darasa hilo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Longido, Simon Laizer amelishukuru shirika la CORDS na wafadhili shirika la Douglas Scott Foundation la nchini Australia kupitia mradi wa Action on poverty. kujenga darasa hilo.

"Darasa hili litasaidia sana vijana ambao hawakusoma katika mfumo rasmi wake hapa kusoma na hivi kupambana na ujinga na umasikini," amesema.

Mkurugenzi wa shirika la CORDS, Lilian Looloitai amesema darasa hilo litakuwa fursa ya pekee kuwasaidia watoto husuani wa kike ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na shule kwa wakati.

Amesema mazingira ya jamii za pembezoni hususani wafugaji wa kimasai zinazokabiliwa na changamoto nyingi ambazo hupelekea watoto kutopata nafasi ya kuanza masomo kutokana na kukosekana madarasa maalum ya Memkwa ambayo huwapelekea kutokuwa na ari ya kuanza kusoma masomo hayo ya elimu ya msingi.

Amesema mwaka 2019 na 2020 walikuwa na mradi wa kuandikisha wanafunzi wa Memkwa wapatao 20 na kuanza kufundishwa shuleni hapo lakini kutokana na kukosa chumba maalum cha kuwafundishia walipelekwa shule ya msingi.

Mkurugenzi wa shirika la Douglas Scott foundation toka Australia, Adrian Scott amesema kuwa wanafurahi kusaidia ujenzi wa darasa hili kwani litasaidia kuondoa ujinga kwa watoto na pia kuwezesha kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa shule hiyo Kwamboka Nyanami Phirace amewashukuru Cords kwa kuwajengea darasa hilo na kuahidi kushirikiana na uongozi wa kijiji kuhamasisha wazazi kuandikisha wanafunzi wa kutosha darasa hilo na wataanza masomo yao rasmi January 2023.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...