SHIRIKA LA Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limebainisha kwamba katika kutekeleza majukumu yake limejikita kwenye kutoa elimu kwa wananchi kufahamu namna linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria

Hayo yalisemwa na Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin wakati wa mahojiano maalumu na mtandao huu katika Maonesho ya tano ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita.

Amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo pia Shirika hilo limeendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho hayo ili kufahamu namna linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.

Alisema kwamba wanashiriki maonesho hayo ya teknolojia na uwekezaji kwenye sekta ya madini yanayofanyika mkoani Geita ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi juu ya majukumu yanayotekezwa Kisheria.

“Lakini kama mdhibiti wa shughuli za usafiri kwa njia ya maji tunasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, tunadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba katika vyombo vya usafiri kwa njia ya maji”

Aidha pia alisema katika maonesho kutoa elimu kwa wananchi wa Geita hususani wadau wa Madini katika jukumu letu la kipekee kwenye biashara ya Meli ambapo kwa sasa wanafanya uondoshaji wa shehena kwa makinikia na mashine zinazotumika katika migodi hivyo wanawakaribisha waweze kupata elimu zaidi itakayowasaidia kujua nini cha kufanya wanapotaka kuagiza mashine zao kuziingiza hapa nchini na kuzitoa pia na usafirishaji wa Makinikia

Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimmizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.

Aidha Shirika hilo pia lina wajibu wa kuhimiza ufanisi, uchumi na uaminifu, kuendeleza upanuzi wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji, kuhimiza ushindani katika biashara ya uwakala wa meli, na kuingia kwenye majukumu ya kimkataba na watu wengine au kikundi cha watu.

Maonesho hayo ya Teknolojia ya Madini ni maonesho ya tano kufanyika Mkoani Geita yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza Teknolojia za kisasa katika sekta hiyo pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo TASAC. 

Afisa Masoko Mwandamizi wa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kalvin (wa kwanza kulia) akikabidhi zawadi Kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Bw. Msafiri Mbibo alipofanya ziara katika kutembelea Banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya tano Teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani Geita.


Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC Martha Kalvin akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wengine wa Taasisi hiyo kwenye Banda lao.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...