Picha ya pamoja wa Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Dar es Salaam , Jeshi la Polisi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)Dk.Edwin Mhede mara baada ya kujadiliana kuhusiana matumizi sahihi ya miundombinu ya Barabara yaendayo Haraka.*Wakuu Wilaya Wakiri kusimamia matumizi ya barabara hizo kwa mifumo ya taarifa kwa Wakala huo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MWENYEKITI wa Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James ameshauri Uongozi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) pamoja na Jeshi la Polisi kutengeneza mifumo ya ndani ya taarifa itakayosaidia kuondoa misuguano wakati wa matumizi ya Barabara za mabasi hayo panapotokea dharula

Aidha amewataka viongozi na watumishi wote wa Umma kutimiza kwa kuzingatia na kuheshimu sheria na taratibu zote za matumizi ya miundombinu ya DART na hivyo kujiepusha na mikono ya sheria kwa kuwa hakuna yeyote aliye juu ya Sheria kwani mradi huo umetumia fedha nyingi.

Ametoa kauli hiyo Oktoba 4,2022 wakati wa kikao cha pamoja cha wadau wa usafiri wa kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na baadhi Maofisa wa Jeshi la Polisi kujadili matumizo sahihi ya barabara ya mabasi yaendayo haraka.

James amesema wakati mwingine dharula haiwezi kutolewa kutokana na mazingira yaliyopo panapotokea watapewa taarifa

"Lengo ni kuhakikisha wote kama wadau muhimu mnakuwa kitu kimoja kusimamia kikamilifu miundombinu ya mabasi yaendayo haraka ili iweze kulindwa, katika kufikia hilo, ninyi kama sehemu ya Serikali mnapaswa kuwa kitu kimoja" Amesema

Aidha kuhusu magari ya Polisi kutumia Barabara hizo, James amesema kwa sasa kinachopaswa kufuatwa ni agizo la IGP Wambura, lakini DART na Polisi Wana kila sababu ya kukaa pamoja na kuona wakati upi magari hayo yatumie barabara za DART.

Amesema zipo nyakati za dharura ambapo magari ya Polisi, zimamoto, gari la wagonjwa ama gari binafsi ambalo ndani yake kabebwa mgonjwa aliyezidia yanapaswa kupewa nafasi ya kupita katika barabara hizo bila kusababisha malumbano

Pamoja na hayo James pia amewataka wananchi kuheshimu matumizi ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka huku akibainisha kuwa asilimia kubwa ya ajali zinazotokea klna kuhusisha mabasi hayo zimesababishwa na wavamiaji.

Hata hivyo amesema kuwa Mtendaji Mkuu Dk.Mhede licha ya changamoto ya matumizi ya barabara kwa baadhi hajawahi kuzungumza kupitia vyombo vya habari bali alitumia nafasi hiyo kutoa taarifa za ndani kwa ndani.


Kwa upande Mtendaji Mkuu wa DART Dkt. Edwin Mhede amesema wao kama DART jukumu lao ni kuhakikisha wanatoa huduma kwa kiwango cha juu na kwa wakati kwa kutumia Barbara zake hivyo chombo kingine tofauti na mwendokasi kupita katika barabara hizo lazima wakinyoshee kidole kwa kuwa sheria pia imeweka wazi

Aidha alisema ushauri uliotolewa na Mkuu wa Wilaya wao kama DART kwao wanauona mzuri kwa kuwa umelenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora za mabasi hayo.

Naye Kamanda Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam William Mkonda amesema kazi ya Jeshi la Polisi ni pamoja na kusimamia miundombinu ya DART liweze kufikiwa na hivyo kutimiza adhma ya Serikali ya kuwekeza katika Barabara hizo ili ziweze kupitika kwa urahisi muda wote kwa magari maalumu.

Amesema kwa wale wachache ambao dhana ya utii wa Sheria bila shuruti kwao bado tatizo, Jeshi hilo linawashughulikia kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa za matumizi ya miundombinu hiyo.

Amesema wanashirikiana vizuri na DART kuhakikisha watumiaji wa Barabara hizo wanafuata taratibu zilizowekwa huku akibainisha kuwa kufanyika kwa kikao hicho ni mwanzo mashirikiano na DART kwa ajili ya maendeleo ya mradi huo.
Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam Kheri James akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) , Wakuu wa Wilaya na Jeshi la Polisi kujadili na kupeana elimu ya matumizi ya Barabara mabasi Yaendayo Haraka , jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Godwin Gondwe akizungumza katika kikao cha matumizi ya barabara ya mabasi yaendayo haraka , jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya Kigamboni  Fatuma Nyangasa  akizungumza katika kikao cha matumizi ya barabara ya mabasi yaendayo haraka na na uhitaji wa usafiri huo kwa wakazi wa Kigamboni  , jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede akizungumza kuhusiana na kikao cha kupeana elimu na wakuu wa Wilaya na Jeshi la Polisi namna bora ya kulinda miundombinu ya Mabasi yaendayo haraka , jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja wa Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Dar es Salaam , Jeshi la Polisi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)Dk.Edwin Mhede na wafanyakazi na Wadau wa DART mara baada ya kujadiliana kuhusiana matumizi sahihi ya miundombinu ya Barabara yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...