Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akiangalia bidhaa ya  sukari inayotengenezwa na kiwanda cha  Bagamoyo Sugar  kilichopo Mkoani Pwani.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza leo mchana wakati alipokua mgeni rasmi katika maonesho ya tatu ya Maonesho ya Uwekezaji ya Biashara yanayoendelea kufanyika Maili Moja Mkoani Pwani.
Picha ya Pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akizungumza na viongozi, wawekezaji  pamoja na wananchi wananchi kwenye uzinduzi wa maonesho ya tatu ya Maonesho ya Uwekezaji ya Biashara yanayoendelea kufanyika Katika Viwanja vya maili Moja Mkoani Pwani.

Na Khadija Kalili, Pwani
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) kutengeneza bidhaa zenye viwango vya ushindani nchini na nje ya nchi.

Dkt. Kikwete amesema haya leo alipokuwa mgeni rasmi katika maonesho ya tatu ya Maonesho ya Uwekezaji ya Biashara ambayo yameanza leo  Oktoba 6 na ameyafungua rasmi mchana  na yanayoendelea kwenye viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

Aidha Rais Mstaafu Kikwete amesema hayo huku akitolea mfano wa bidhaa za mashine zilizotengenezwa na SIDO ambazo ni za kubangulia korosho kuwa hakuridhishwa na ubora wake wa utengenezwaji pamoja na umaliziaji wake kuwa haziwezi kuhimili ushindani sokoni.

Amesema kuwa hivi sasa ushindani wa mauzo ya bidhaa sokoni ni mkubwa hasa ikizingatiwa nchi ni mwanachama wa nchi za Afika Mashariki ambapo katika nchi jirani wametuzidi

"Nachukua fursa hii kuwaasa SIDO kupambana na ushindani wa bidhaa mnazozitengeneza na kuzisimamia kwa kujali ubora wake kabla ya kupeleka sokoni na kuzingatia kumudu ubora wa bidhaa ili kukabiliana na ushindani wa soko la biashara kwani hivi sasa soko ni huru katika nchi za Afrika na dunia nzima."

"Mnaanzisha shughuli za viwanda hakikisheni ubora wa bidhaa mnazozizalisha vinginevyo itakula kwetu kwani bidhaa zetu zitakosa soko" amesema Dkt.Kikwete

Dkt. Kikwete amesema kuwa ubora wa bidhaa ni muhimu na tusitengeneze bidhaa za kibongobongo kwa sababu hata hata wabongo wanahitaji bidhaa bora.

Aidha Dkt. Kikwete ametoa rai kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge kuweka mipango mkakati wa kutenga maeneo makubwa ya Kongani ya viwanda ambayo hayatakujakuleta madhara katika miaka ijayo huku akitolea mfano maeneo ya ujenzi wa viwanda Wilayani Mkuranga jinsi ujenzi holela wa viwanda huku akisema pindi serikali itakapohitaji kufanya upanuzi wa barabara viwanda vingi vitaathirika kwa sababu vimejengwa karibu na barabara.

"Nawaasa tengeni maeneo makubwa ya viwanda hata kama yatakuwa yako nje ya mji ili kuweza kunusuru makaaI ya watu hapo baadaye jitengenezeeni mipango mizuri ya maendeleo na uwekezaji mfano mzuri ni namna mlivyoutenga mji mpya wa bandari kavu ya kwala ambapo Kongani hiyo ina ukubwa wa ekari 2 500 .

Wakati huo huod Kikwete  Dkt.amesema kuwa ni muhimu kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani uka ukaweka utaratibu wakupima viwanja kwa ajili ya watu wa hali ya chini "uzuri nyumbani kwangu naishi na Naibu Waziri wa Ardhi hivyo nitamwambia kuwa pimeni viwanja vya bei nafuu ili wananchi wa hali ya kawaida wanaoishi katika eneo la Kwala waweze kumudu kumiliki ardhi katika eneo hilo ambalo linatatajiwa kua mji mkubwa wa biashara na pia pajengwe mji mzuri na wakisasa" alisema Kikwete.

Maonesho haya yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kushirikiana na SIDO ambapo wawekezaji 200 wanashiriki wa Maonesho haya yamedhaminiwa na SINO TAN ambao ndiyo wadhamini wakuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...