MKUU Wa Majeshi Ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda ameahidi kukuza mchezo Wa Gofu Na Kuboresha Shindano La Mkuu wa Majeshi La CDF TROPHY lililofanyika Kwenye klabu ya Jeshi Lugalo Gofu Jana, Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Kwenye Halfa Ya Kufunga shindano hilo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania Jenerali Jacob Mkunda Amesema CDF TROPHY ni shindano la Gofu lenye lengo la kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Jeshi La Wananchi Wa Tanzania-JWTZ hatahakikisha Shindano hilo linafanyika kwa ukubwa zaidi.

"Nitahakikisha naboresha mashindano hayo ili kusherekea vizuri, pia pongezi kwa wadhamini ambao wamesababisha mashindano haya yanafanya vyema."

Pia amelishukuru jeshi la Malawi kuhudhuria shindano hilo na kupokea mualiko wao katika kukuza mchezo huo kwa nchi ya Malawi.

Kwa upande wake Jenerali Vicent Nundwe Mkuu wa Majeshi wa Malawi Amesema shindano hilo kubwa lenye kudumisha umoja na mshikamano kwa mataifa hayo kupitia mchezo wa Gofu huku akiahidi kufanyia kazi yale mazuri aliyoyaona kutoka jeshi la Tanzania.


"Nimejifunza vingi hivyo natamani hata wadhamini ambao wamejitokeza waweze kuja nchi Malawi Ili tuone Kwa namna gani na sisi tunafanya Mashindano kama haya kwa ukubwa Ili kuwapa moyo wachezaji wa mchezo wa gofu."

Mwenyekiti wa klabu Ya Jeshi Lugalo Gofu Brig.Jenerali Michael Luwongo amemshukuru Mgeni Rasmi Jenerali Jacob Mkunda Mkuu Wa Majeshi kwa kukubari Uwito huo pamoja na wadhamini wote kwa mchango wao kuweza kufanikisha shindano hilo kubwa la kihistoria hususani Benki ya NMB.

"Pongezi kwa NMB kwa kujali vipaji vya vijana mahitaji mengi kama klabu mengine tunashindwa, tunaamini vifaa hivyo ambavyo vitanunuliwa vitakuwa chachu ya watoto kuongeza juhudi katika mchezo huu".

Mchezaji Malius Kajuna mshindi wa jumla wa shindano la" NMB CDF TROPHY 2022" kutoka klabu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania-JWTZ, Amesema Ushindani ulikuwa mkubwa Licha ya Kuibuka na ushindi huo.

"Nashukuru wadhamini wote walikuwepo kuhakikisha mashindano haya yanafanyika wao ndiyo chachu ya sisi kufanya vizuri, pia pongezi kwa kunipa wakati ngumu".

Wachezaji wengine walioibuka na ushindi kwenye shindano la NMB CDF TROPHY 2022, Overall winner Net Onestery Mhalwike,Washindi Divisheni A,Sam Kileo Mikwaju 143 na Arudo Gandye mikwaju143, Divisheni B,D.Seth Mikwaju 139 na Khalid Shemndolwa Mikwaju 143, Divisheni C,John Idd Mikwaju 150 na Faimu Mbaraka Mikwaju 151, Kwa upande wa Wanawake Ladies Gross Angel Eaton Mikwaju 157,Ladies Winners, Khadija Lusakale Mikwaju 139,Zanura Mohammed Mikwaju 139,Zainabu Ibrahim Mikwaju 142,Habiba Sanze Mikwaju 143, wachezaji wa kulipwa Pro Abdallah Yusuf akifatiwa na Pro.Fashil Nkya wote kutoka Lugalo Gofu.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania Jenerali Jacob Mkunda kulia kwake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Malawi Jenerali Vicent Nundwe kulia kwake Muwakilishi kutoka Benki ya NMB Huku kushoto kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania akiwemo Mkuu wa Majeshi mstaafu George waitara pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo gofu Brig.Jenerali Michael Luwongo,Mshindi wa Jumla wa Shindano hilo Malius Kajuna pamoja uongozi wa Benki ya NMB ambao ndio wadhamini wakuu katika Shindano la CDF TROPHY 2022 lililofanyika katika viwanja vya gofu Lugalo jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...