Kaimu Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), Khassim Musya akitoa elimu wa wananchi waliofika katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani  yenye Kaulimbiu isemayo 'Uzalishaji bora, Lishe bora, Mazingira bora na Maisha bora kwa wote, Habaki Mtu Nyuma.
MADHARA ya ulaji wa sumu Kuvu husababisha  kupungua kwa kinga ya mwili, kushuka kwa uzalishwaji wa maziwa na mayai, upungufu wa damu, Kukosa hamu ya kula, kuharibika kwa mimba, Kuathiri mfumo wa uzazi, Kuharisha, Kutapika na Vifo.       

Hayo yameelezwa na Kaimu Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), Khassim Msuya katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani  yenye Kaulimbiu isemayo 'Uzalishaji bora, Lishe bora, Mazingira bora na Maisha bora kwa wote, Habaki Mtu Nyuma' ambayo yanafanyika mkoani Simiyu. Amesema Sumukuvu zinapokuwepo kwenye mazao au bidhaa hazionekani kwa macho, na kwamba huendelea kubaki hata baada ya chakula kupikwa au kusindikwa.

Madhara hayo ya sumukuvu huweza kujitokeza ndani ya muda mfupi, baada ya muda mrefu kutegemea na kiasi 

cha sumukuvu hiyo iliyopo kwenye chakula kilicholiwa, idadi ya milo ya chakula kilichochafuliwa na umri pamoja na hali ya afya ya mlaji.

"Mazao yanayochafuliwa na kuvu ni kama vile nafaka (mahindi, mtama, ulezi, mchele, ngano, uwele), mbegu za mafuta (alizeti, pamba), karanga, korosho, jamii ya mizizi iliyokaushwa (mihogo na viazi), viungo vilivyokaushwa, kahawa, mazao yanayotokana na mifugo (maziwa, mayai)." amesema Msuya.

Dalili zinazoashiria kuwa mazao yamechafuliwa na kuvu wanaozalisha sumukuvu ni pamoja na ukungu, kuvu, harufu ya uvundo, punje kutengeneza vumbi, punje kugandamana au punje kubadilika rangi na kuwa na rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu, kijani, chungwa au njano.

Amesema athari za sumukuvu kiuchumi ni kukataliwa kwa bidhaa za chakula katika soko la ndani na nje ya nchi, Kuathiri utoshelevu wa chakula, kuathiri uzalishaji wa mifugo, kuongezeka kwa gharama za matibabu, kupungua kwa nguvu kazi na uzalishaji mali na kuongezeka kwa gharama za udhibiti.

Vichochezi vya uchafuzi wa sumukuvu kwenye mazao ya chakula na uwepo wa mazingira wezeshi kwa kuvu kuota na kuzalisha sumukuvu ni pamoja na hali ya hewa, joto-ridi (temperature), unyevunyevu, ukame, mafuriko na mvua zisizotarajiwa wakati mazao yanapokaribia kukomaa na wakati wa kuvuna.

Amesema inashauriwa mkulima kutumia mbegu zenye ukinzani dhidi ya magonjwa au zile zinazoweza kustahimili hali ya mazingira ya shamba husika.

Pia mkulima anashauriwa kwa kadiri inavyowezekana kubadilisha mazao kwa mzunguko kati ya yale yanayoathiriwa na yasiyoathiriwa na kuvu, Mfano kupanda mahindi msimu mmoja na jamii ya mikunde msimu unaofuata.

Akizungumzia mafanikio ya TANIPAC, Mratibu huyo amesema hadi sasa wakulima 61,410 wamepatiwa elimu juu ya udhibiti wa sumukuvu baada ya mavuno ambapo lengo lilikuwa ni kuwafikia wakulima hao  60,000.

"Kwa upande wa vijana  tumewawezesha vijana 420 kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wamejengewa uwezo kwenye kutengeneza Vihenge chuma (Metal silos) ambayo ni mbinu ya kuzuia mazingira wezeshi ya ukuaji wa kuvu, lengo lilikuwa 400 pamoja na Maafisa ugani 1,351 na Wanahabari 217,"alisema Msuya.


Mratibu huyo amefafanua kuwa tulifundisha vijana 420 na sasa tunawafanyia program atamizi Kwa Kuwafundisha maswala ya ujasiriamali ili waweze kutengeneza vihenge kibiashara. 


Mratibu huyo ameeleza kuwa lengo ni kutengeneza vihenge 10,000. Mradi utapromote vihenge kuhusu hiyo technolojia na kueajulisha wananchi na kuweza kuwapa fursa ya kutengeneza vihenge hivyo.


Amefafanua kuwa  mradi  huo wa TANIPAC ni wa miaka mitano  ambapo ulianza mwaka 2019  na yanatarajiwa kukamilika mwaka  2024, ambao unaotekelezwa Tanzania Bara na Visiwani – Zanzibar (Unguja na Pemba).

Mratibu huyo ameongeza kuwa pamoja na changamoto ya COVID -19 lakini  wananchi, taasisi na Wizara tayari wanauelewa wa  madhara ya Sumukuvu huku  akitolea mfano Wizara ya Mifugo na uvuvi wameomba kupatiwa elimu ya sumukuvu.

Siku ya Chakula Duniani huadhimishwa Oktoba 16, kila mwaka katika nchi zipatazo 150 ikiwamo Tanzania.

Lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu Usalama wa Chakula, utambuzi na usimamizi wa athari zitokanazo na chakula pamoja na kuboresha afya za binadamu kupitia utoaji wa elimu hiyo.

[09:20, 10/17/2022] Avila: Shirika la Chakula na Kilimo na Umaja wa Mataifa (FAO), na serikali ya Tanzania kupitia program inayo na Umoja wa Ulaya Agree Connect imegundua kampeni ya kitaifa ya 'Lishe Bora ni Mtaji' ili kujenga tabia ya zinazofaa za milo hapa nchini kwa kutumia vyakuka vinavuopatikana Tanzania.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...