Na Munir Shemweta, WANMM SHINYANGA 

Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Anthony Mavunde ametoa rai kwa watendaji wa serikali kuhakikisha yale maeneo yote ambayo migogoro ya ardhi imetatuliwa yanapangiwa mipango ya matumizi ya ardhi kwa kujumuisha maeneo ya mashamba makubwa ya kilimo badala ya kupanga maeneo ya makazi tu peke yake.

 

Naibu Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo jana wàkati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lyamidati mkoani Shinyanga wakati Kamati ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta wanaoshughulikia migogoro ya matumizi ya ardhi ya vijiji 975 walipofika eneo hilo.

 

"Nitoe rai yale maeneo ambayo migogoro yake ya matumizi ya ardhi imetatuliwa basi iwekewe matumizi bora ya ardhi   ili mashamba makubwa yasisahaulike na wakulima wapate maeneo ya kutosha walime mwisho wa siku waisaidie nchi kukuza uchumi wao mtu mmoja mmoja,uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla’’. Alisema Mavunde

 

Badala ya maeneo ambayo utatuzi wake umefanyike kutengwa kwa ajili ya makazi peke yake ni lazima wataalamu wasimamie mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kuhakikisha wanaingiza maeneo makubwa ya mashamba ya kilimo kwa sababu. Mh Rais Samia Suluhu Hassan amekuja na mpango wa kuwa na mashamba makubwa ya pamoja (block farms) ili kusaidia kukuza sekta ya kilimo kufikia malengo yake ya kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

 

Kwa mujibu wa Mavunde mashamba hayo makubwa ya pamoja yatasaidia kurahisisha utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima hasa katika mbinu bora za kilimo cha tija na usambazaji wa teknolojia mbalimbali za kilimo ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo.

 

‘’Serikali ina mpango wa kuwa na mashamba makubwa ya pamoja 10000 kufikia mwaka 2030 na kwa sasa sasa hivi nchi nzima ina jumla ya mashamba makubwa ya pamoja zaidi ya 110

 

Kamati ya Mawaziri nane wa Wizara za kisekta iko katika ziara ya kutembelea mikoa mbalimbali kwa lengo la kutoa mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhususiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 na tayari katika awamu hii ya pili kamati hiyo imeshatembelea mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma, Simiyu na Shinyanga.Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Lyamidati Mkoani Shinyanga wakati kamati ya mawaziri 8 wa kisekta wanaoshughulikia migogoro ya Ardhi ya Vijiji 975 walipofika katika eneo hilo jana.aibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wananchi katika kijiji cha Lyamidati Mkoani Shinyanga wakati kamati ya mawaziri 8 wa kisekta wanaoshughulikia migogoro ya Ardhi ya Vijiji 975 walipofika katika eneo hilo jana.Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta katika kijiji cha Lyamidati ShinyangaNaibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akiwa na timu ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Lyamidati Shinyana wakati kamati ya mawaziri 8 wa kisekta wanaoshughulikia migogoro ya Ardhi ya Vijiji 975 walipofika katika eneo hilo jana. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...