MICHUANO Shirikisho la Michezo ya Wiraza na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) imezidia kurindima katika viunga vya jiji la Tanga ambapo Timu za Kamba za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zimeendeleza ubabe wao kwa timu za kundi E wanaume na kundi F Wanawake.

Katika michezo ya leo Oktoba 4,2022 timy ta Kamba ya Uchaguzi wanaume wamewahenyesha na kuchukua lama tatu kutoka kwa Mhimili wa Bunge.

Mchezo huo ambao awali ulikua unaonekana kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na aina ya wachezaji waliopo lakini ulikuwa mwepesi kwa miamba ya Uchaguzi.

Katika mchezo mwingi Timu ya wanawake wa Uchaguzi ilipata alama tatu za mezani kufuatia wapinzani wao RAS Ruvuma kuingia mitini katika mchezo wa kundi F.

Baada ya matokeo hayo sasa Timu ya Wanawake wa Uchaguzi imebakiza mchezo dhidi ya Wizara ya Madini ambapo wanaume wanasubiri kukutana na RAS Shinyanga.

Kundi la Kamba wanaume lina timu za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, RAS Shinganga na RAS Manyara.

Upande wa Kundi F timu ya Kamba wanawake kuna timu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, RAS Dodoma, RAS Ruvuma na Wizara ya Madini.

Timu ya Kamba wanaume ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kiwavuta Timu ya Kamba ya Bunge (hawapo pichani) wakati wa Michuano Shirikisho la Michezo ya Wiraza na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) inayoendelea jijini Tanga. Timu ya Uchaguzi ilishinda mchezo huo kwa mivuto yote miliwi. (Picha na Mroki Mroki).




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...