Na MWANDISHI WETU
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amewahakikishia wanachama, waajiri na wadau kuwa Mfuko utaendelea kutoa huduma bora na endelevu kwa kuzingatia dira na maadili.

Mshomba amesema hayo leo tarehe 3 Oktoba 2022 katika Ofisi za NSSF Ilala na Temeke katika jengo la Mafao House wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2022 yenye kauli mbiu isemayo “Huduma Bora Kipaumbele Chetu”.

Mshomba amesema Wiki ya Huduma kwa Wateja ni muhimu kwa sababu Mfuko unapata nafasi ya kuwatambua watumishi wanaotoa huduma na pia kuwatambua wateja ambao amewahakikishia kuwa wataendelea kuboresha huduma kwa wateja kwani bila ya uwepo wa wateja hakuna Mfuko.

“Nashukuru tumepata nafasi ya kukutana na wateja wetu ambapo tumewahakikishia kuwa tutaendelea kutoa huduma endelevu, zilizo bora kwa kuzingatia dira na maadili ya Mfuko,” amesema Mshomba.

Mshomba amesema wametumia maadhimisho hayo kueleza mafanikio ambayo Mfuko umeyapata katika mwaka wa fedha 2021/22, hasa katika makusanyo, uandikishaji wanachama na uboreshaji wa mifumo ya taarifa zikiwemo huduma za taarifa kiganjani, mifumo ya upatikanaji wa taarifa za wanachama na waajiri kwa njia ya kielekitroniki ambazo zinarahisisha kulipia michango ya wanachama, kupata taarifa za wachangiaji na uwasilishaji wa michango bila kufika katika Ofisi za NSSF.

Amesema hivi sasa Mfuko umejikita katika utoaji elimu kwa wanachama, wateja na wadau wengine lengo ni kuhakikisha umma wa Watanzania wanafahamu hifadhi ya jamii, mafao yanayotolewa na NSSF na huduma zinazotolewa na Mfuko ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi hasa yanayohusu mafao yao katika Mfuko.

Mshomba amesema mojawapo ya vipaumbele muhimu sana ni kuweka mifumo ya TEHAMA lengo ni kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora popote walipo kwani bila ya kuweka mifumo hiyo suala la huduma kwa wateja halitafikia viwango ambavyo Mfuko unatarajia kuvifikia.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...