Na Karama Kenyunko Michuzi TV
 
KAMPUNI ya simu ya Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya Smart Codes Accelerator imewatangaza washindi 13 wa programu ya kuibua vipaji vya ubunifi wa kidigitali kwa vijana wa kitanzania.

Kampuni hizo zitawapa wabunifu hao misaada mbali mbali kubwa ikiwa kukuza mawazo yao ili kuwa miradi mikubwa nchini.

Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa huduma za kidigitali kutoka Vodacom Nguvu Kamando amesema kuwa wabunifu wadogo watapatiwa mafunzo usimamizi na msaada kwa muda wa wiki 13 ili kuwawezesha kuwafanya mawazo yao kuwa bora na yenye tija kwa jamii.

Amesema, katika Programu hiyo mawazo kutoka kwa wabunifu 300 yalipokelewa katika maeneo ya Kilimo, Afya, Vyombo vua Habari , Elimu na Biashara ya Mtandaoni ambapo baada ya mchujo wabunifu 13 wakaibuka kuwa washindi.

Washindi hawa wa leo tutakuwa nao kwa wiki takribani 13, tukiwapika ili wakitoka hapo walete matunda kwenye ulimwengu wa matunda wa kidigitali.... kwani mawazo mengi yanayochaguliwa ni yale yanayokwenda kutatua matatizo kwenye elimu, Afya, huduma za kifedha, usafirishaji, kilimo, Ulinzi kwenye mitandao nk. Amesema Kamando

Amesema kuwa wabunifu hao watapata usimamizi kutoka kwa wataalam ambao ni wafanyakazi wa Vodacom na Smart Lab na wanataaluma wengine.

“baada ya Miezi Mitatu wabunifu hawa wataweza kutengeneza bidhaa zao na kwamba wabunifu watatu hodari zaidi watapata awamu nyingine itakayowajengea uwezo zaidi kwa kuwasaidia kwenye soko la Kimkakati kuwashika mkono kwenye biashara, na kuwapa mtaji"

Watapatiwa technical, business msaada wa Kiteknolojia na ubunifu kwa ajili ya kuwakuza kutoka Smart Lab" amesema.

Amewataja waliochaguliwa kwa mawazo bora ya ubunifu ni Shule Yetu Innovation , Smart Darasa, Lango Academy Lango Academy, Vijana Tech, Hack it Consultancy, Seto, Twenzao, Get Value, Spidi Africa, Dawa Mkononi, Medpack, Bizy Tech and Bizzy Pay.

Kwa upande wake, Ofisa Rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Vivienne Penesis, amesema Vodacom imeanzisha Programu nyingine inayoitwa “Code Like a Girl” ambayo inalenga kuwapa nguvu wanasichana kwenye kwenda mbali zaidi na kuongeza thamani kwenye ujuzi wa kidigitali na kuwa na tafakuli pana.

Amesema mpaka sasa programu hiyo ishameisha wanufaisha wanasichana 1,444 ambao wanaingiza kipato na kwa kusimamia tovuti (Website) zinazowaingizia kipato.

Naye Edwin Bruno, Mkurugenzi Mkuu wa Smart Codes Africa Group amesema ataendeleza programu hiyo yenye matokeo chanya kwenye jamii ambapo wabunifu wataweza kuongeza thamani kwa kuwashawishi wawekezaji.

“tutaendelea kuwa sehemu ya huu mradi kwa matumaini ya kuwatengenezea daraja la kibunifu kwa vijana ili kujijenga kijasiliamali kibiashara na kibunifu.

"Tutawatafutia wawekezaji watakaoweza kuwapatia ufadhili ama pesa ili waweze kuhakikisha ile mchakato ya mawazo yao inakuwa kwa haraka zaidi bila kukwama na pia tunawasaidia kukuza yale mawazo yao yasifanye tu kazi Tanzania bali yaende hata nje ya Afrika na duniani kote". Amesema Bruno.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...