Na WMJJWM, Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima, amewaomba wazee kubadilisha hadithi za kale walizo wasimulia wajukuu zao kuhusiana na Imani za kishirikina na badala yake wakawahadithie hadithi zitakazowajenga na kuwa raia wema kwa taifa.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo Oktoba 02, 2022 wakati wa Kongamano la Wazee kuelekea Kilele cha Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa, zipo baadhi ya Jamii, wakiona mzee macho yamekuwa mekundu na yanatoa Machozi na wengine wamezeeka na Migongo kupinda huibuka na dhana kuwa ni washirkina jambo ambalo sio la kweli hivyo nilazima tubadili fikra hizo kwa sasa.

"Wazee wangu niwaombe sana, kama kuna baadhi yenu waliwahi kuwahadithia wajukuu juu ya Habari za kishirikina huko nyuma na kuchochea Vitendo vya Ukatili basi ni wakati wa kuwabadili Fikra kwa kuwapa hadithi zitakazo wafanya kuwa Raia wema kwa Taifa lao" alisema Dkt. Gwajima

Ameongeza kuwa kwa sasa Serikali inaendelea kuwasuka SMAUJATA waendelee kuwa wengi watakaofika hadi ngazi ya Kijiji na Kata aidha kwaupitia Maafisa ustawi na Maendeleo Jamii mifumo yao iendelee kufanya kazi ya kufichua na kutokomeza Vitendo vya Ukatili kwa Makundi yote ikiwepo Wazee.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Lameck Sengo ameiomba Serikali kuona suala la kuwashirikisha kwenye vyombo vya maamuzi linatekelezwa kwani kuwepo na uwakilishi katika vyombo hivyo husaidia wazee sauti yao kusikika.

"Katika Sensa ya 2012 sisi Wazee tulikuwa Milioni 2.5 na tunaimani kwenye Sensa ya Mwaka huu tutaongezeka zaidi kutokana na Serikali yetu kutuboreshea huduma zetu hivyo kama Baraza la Wazee limekamilika ni wakati muafaka sasa kupata uwakilishi katika vyombo vya maamuzi." alisema Mzee Lameck.

Awali Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bibi Amina Mfaki amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za Wazee ikiwepo kuwepo kwa madirisha ya Wazee kwenye maeneo ya kutolea huduma za Afya sambamba na upatikanaji wa Vitambulisho vya msamaha wa Matibabu kwa Wazee pamoja na wengine kukatiwa Bima ya Afya ya jamii.

"Zaidi ya Wazee Millioni 2.1 wametambuliwa na zaidi ya Wazee 500,000 wamepatiwa vitambulisho vya Bima ya Afya" amesema Bibi Amina.

Siku ya Wazee Duniani hufanyika kila Mwaka Oktoba Mosi na kwa Mwaka 2022 Maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Kaulimbiu isemayo "Ustahimilivu na Mchango wa Wazee ni Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa".
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na Wazee kwenye Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Amina Mfaki akitoa salam za Wizara hiyo wakati wa Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la l Wazee Lameck Sendo akitoa salaam za Wazee wakati wa Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Wazee wakati wa Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akikagua huduma za Afya zinazotolewa kwa Wazee wakati Kongamano lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Baadhi ya Wazee walishiriki kwenye Kongamano kueleke Siku ya Wazee wakiwa wanafuatilia mada mbalimbali wakati Kongamano lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na Wazee wakati wa wakati wa Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...