Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampuni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Amani visiwani Zanzibar utakaofanyika Desemba 17, 2022.

Kampeni hizo zimezinduliwa leo Alhamisi, Desemba 1, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ambapo pamoja na mambo mengine, amemnadi mgombea wa chama hicho, Abdul Yussuf Maalim.

Katika uzinduzi huo, Shaka amewataka wananchi wa jimbo hilo kuchagua mgombea iliyemsimamisha na CCM kwa kuwa ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi CCM.

Amebainisha kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi anaendelea kufanya kazi kubwa na nzuri, hivyo anastahili kupewa viongozi atakaoshirikiana nao katika kwatumikia wananchi kwa kuhakikisha kasi ya kuletea maendeleo iliyoanza inakamilishwa kulekea 2025 ili CCM iendelee kuaminiwa kwa kipindi kingine.

Aidha, amefafanua kuwa kazi ya kuleta maendeleo hususan katika jimbo hilo haiwezi kuletwa na kila mtu, hivyo kuna kuna umuhimu mkubwa wa kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM ili atimize wajibu huo kwa watu wa jimbo hilo.

“Kazi ya kuleta maendeleo ya nchi hii hapewi kila mtu, kazi ya kuleta maendeleo jimbo la Amani sio kila mmoja anaweza kuleta maendeleo, wapo wenye uwezo wa kuleta propaganda kwenye jimbo la Amani ”

“Lakini wapo wenye uwezo wa kuleta maendeleo wana amani mkasema kweli haya ni maendeleo ambayo tunayahitajia, ndiyo maana tukasema Abdul songa mbele nenda ukapeperushe bendera ya Chama Cha Mapinduzi nawahikisha ataifanya kazi hii kwa uweledi na ustadi wa hali juu” amesema Shaka

Mapema Shaka aliwakumbusha wananchi juu ya kazi nzuri iliyofanywa na Rais Samia na Rais Mwinyi katika kipindi cha miaka miwili ni kubwa, ya kutukuka na kupewa huko hivyo wanastahili kupongezwa na kuungwa mkono ikiwamo kumchagua mgombea huyo wa CCM ili kushirikiana katika kuwaletea wana Amani maendeleo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM ndugu Abdul Yussuf Maalim katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika Jimbo la Amani Zanzibar.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Amani Zanzibar, Abdul Yussuf Maalim katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM katika uchaguzi huo.

Baadhi ya Wafuasi na Wanachama cha CCM wakishangilia jambo wakati Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho ndugu Abdul Yussuf Maalim katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM uliofanyika leo katika Jimbo la Amani, Zanzibar.Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza mbele ya mamia ya watu (hawapo pichani) wakati akimnadi mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Amani Zanzibar, Abdul Yussuf Maalim katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM uliofanyika leo mjini humo.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Amani Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Abdul Yussuf Maalim alipokuwa akijinadi na kuomba kura kwa wanachama na wananchi waliofika katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za chama hicho zilizofanyika leo mjini humo. 
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...