Na Mwandishi Wetu,Same

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo ameshiriki kikamilifu kampeni ya kitaifa ya chanjo ya polio awamu ya nne katika Hospital ya wilaya hiyo huku akisisitiza umuhimu wa watoa huduma za ya chanjo hiyo kutoa elimu kwa kila kaya kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo.

Aidha amewataka a wazazi na walezi wenye watoto walio na umri chini ya miaka mitano wajitokeze hili watoto wao wapate chanjo hiyo na kuwakinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio)

Akizungumza kwenye Kampeni hiyo ya chanjo ya Polio ,Mpogolo ametumi nafasi hiyo kueleza umuhimu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kupata chanjo ili kuwa na Taifa lililosalama kiafya na kuepukana na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same Dk Alex amesema timu ya wataalamu ambayo wanatoa huduma ya afya ya chanjo ya polio imesambaa karibu vijiji vyote kutoa elimu kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio) huku wakiakikisha mtoto chini ya umri wa miaka mitano anapata chanjo hiyo

Aidha Mratibu wa Chanjo wilaya ya Same Pilula amesema hospital ya wilaya ya Same imejipanga kikamirifu kuakikisha zoezi hili la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano linakamilika na kuakikisha kila mtoto anapata chanjo hiyo.

Mmoja wa wazazi ameshukuru kwa juhudi kubwa za viongozi wa wilaya ya Same pamoja na watoa huduma wa chanjo ya polio. kuwa kazi wanayoifanya kuakikisha watoto wao wapo salama, na kuwataka wazazi wengine wasiwafiche watoto na kuwa na imani potofu juu ya chanjo hiyo inayotolewa nchi nzima.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...