Na Mwandishi Wetu, Kisarawe

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Nickson Simon wamefanya mdahalo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo pia wameazimia kuendeleza mambo matano muhimu katika kuleta maendeleo ya wananchi.

Akizungumza leo Desemba 9,2022 kwenye mdahalo huo ambao pia ulihusisha ukatakaji wa keki kama ishara ya kusherehekea miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika , Simon amesema wanatambua nafasi ya midahalo ambayo imekuwepo tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere , pia viongozi wa ngazi mbalimbali wamekuwa wakishiriki kwenye kufanya midahalo.

“Kufanya mdahalo katika ngazi ya Wilaya ni kuendeleza utamaduni wetu , lakini nimechagua mada ambazo zilikuwa ni muhimu.Tumezungumza kuhusu utamaduni na maendeleo, siasa na maendeleo wakati kitaifa tumekuwa na utamaduni ambao umetufanikisha sana utamaduni kuwa na umoja, utamaduni kuwa na amani , utamaduni wa kuamini kwamba sisi ni ndugu Tanzania, utamaduni wa Tanzania kuwa na mahusiano mazuri na majirani zake , utamaduni wa mahusiano na mataifa mengine ambao ni muhimu kuutambua, kuutunza.

“Pia tuna tunu za kufanya kazi kwa bidii , kujifunza lakini tuna utamaduni wa kimakundi kama kama Wazaramu , kama Wachaga na makundi mengine. Kuna utamaduni wa mtu binafsi na tumekubaliana vitu kama vitano ambavyo ni muhimu katika kupiga hatua za kimaendeleo,”amesema Simon.

Ametaja mambo muhimu ambayo wamekubaliana kwenye mdahalo huo ni elimu, maarifa, kujituma, uadilifu, nidhamu, na ujasiriamali .“Kwa hiyo katika ni muhimu , bidii, uadilifu , kujituma ni muhimu, ujasiriamali ni muhimu kwa hiyo katika miaka 60 ya Tanzania inayokua mbele tunaamini tukiwa watu wenye elimu , maarifa , bidii , nidhamu na wajasiriamali tunakubali kwamba hivyo ni vitu vya kiutamaduni ambavyo vitatupeleka mbele zaidi.

“Pia tumekubaliana sisi ni watu ambao tunajifunza kutoka kwa wengine ,kwa hiyo tutaendelea na utamaduni wa kujifunza , lakini tumejifunza umuhimu wa siasa na mchango wake kwenye maendeleo na tumekubaliana siasa ambazo haziweki mbele maslahi ya binafsi, bali zinazoweke mbele maslahi ya umma, siasa zenye matokeo chanya.

“Tukiwa na sera ambazo zinajenga kuinua watu inakuwa ni sere yenye matokeo, tukiwa na majadiliano yasiyokuwa na chuki ni matokeo mazuri.Lakini tulikuwa na mjadala uliohusu ukatili wa kijinsi na tumeona takwimu mahusiano kwenye ndoa na tala, hivyo tumekubaliana kuendelea kuboresha mahusiano, kwa mfano ukiweka ahadi ya kumuheshimu mwenza wako, ahadi ya kumsikiliza,”amefafanua.

Pamoja na hayo amesema leo ndio kilele cha kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Taifa letu lakini kabla ya mdahalo huo kuanzia Desemba 1 wamekuwa na matukio mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya kufanya usafi na kupanda miti na jana(Desemba 8) wametoa kadi za bima ya afya 78.“Shughuli zote ambazo tumezifanya kuanzia Desemba 1 hadi Desemba 9 kwa ujumla wake zinalenga kujenga utaifa wetu.Hvyo tunaposherehekea miaka 61 ya uhuru tunajivunia kuendeleza tamaduni zetu.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe alitumia nafasi hiyo kueleza maendeleo makubwa yaliyofanyika ndani ya wilayo tangu nchi ilipopata uhuru wake huku akielezea miaka ya nyuma ambavyo kulikuwa na changamoto mbalimbali lakini Serikali imefanikiwa kuziondoa kwa kiasi kikubwa.

Awali mmoja ya wazee wa wilaya ya Kisarawe ambaye anaishi eneo la Kibaoni Abdallah Majayo alisema amefurahishwa na majadiliano yaliyokuwa yakiendelea lakini anaipongeza hatua za kimaendeleo ambazo zimefanyika wilayani Kisarawe.




Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Nickson Simon (kushoto), Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mwanana Msumi (katikati) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe(kulia) wakiwa wameshika keki kama ishara ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa nchi yetu.Keki hiyo ilikatwa na kulishwa viongozi mbalimbali pamoja wananchi walioshiriki kwenye Mdahalo ulioandaliwa na Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali.



Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kisarawe Eva Stesheni(kushoto) akiweka vijiti kwenye vipande vya keki.Katikati ni Mkuu wa wilaya hiyo Simon Nickson akitoa maelezo kuhusu keki hiyo na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe.



Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon(kushoto) akimlisha keki Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mwanana Msumi(kulia) kama ishara ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika.Tukio hilo la kukata keki limefanyika baada ya kumalizika kwa mdahalo ulioandaliwa na Mkuu wa wilaya hiyo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali wakati wakiadhimisha siku hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon(kushoto) akimlisha keki Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Zeuberi Kizwezwe.Kisarawe imeadhimisha siku ya Uhuru kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kuanzia Desemba 1 na leo Desemba 9 wamehitimisha kwa kufanya mdahalo ngazi ya wilaya.




Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Zuberi Kizwezwe akizungumza wakati wa Mdahalo uliondaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya kiutamaduni wakati Taifa likiadhimisha miaka 61 ya uhuru wake

Ofisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mwandili Rangi akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya mahusiano ya kwenye ndoa ndani ya Wilaua hiyo wakati wa mada ya kuzungumzia mahusiano na unyanyasaji wa kijinsia.Wengine kwenye picha hiyo ni Mkuu wa wilaya hiyo Nickson Simon(katikati) na Kamanda wa Polisi Eva Stesheni (kulia).








Baadhi ya washiriki wa mdahalo uliondaliwa na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Simon Nickson ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wan chi yetu ambapo kwenye mdahalo mada mbalimbali zilijadiliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...