Na Mwandishi Wetu Michuzi TV - Gairo

CHAMA CHA Mapinduzi ( CCM) kupitia Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo kimetoa maelekezo kwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuratibu na kuangalia uwiano wa walimu ili wapelekwe kwenye maeneo yenye uhitaji.

Kwa mujibu wa Chama hicho takwimu zilizopo zinaonesha maeneo ya Mjini kuna walimu wengi kuliko maeneo ya vijijini hivyo ni muhimu kwa TAMISEMI kuweka uwiano sawa wa walimu ili kuondoa tabaka lililopo ambalo likiachwa litasababisha maeneo ya Vijijini kuwa na uhaba wa wasomi.

Akizungumza mbele ya wananchi na Wanachama wa CCM leo Wilayani Gairo mkoani Morogoro Katibu Mkuu wa Chama hicho,Chongolo amesema Wilaya ya Gairo kunachangamoto ya uhaba wa walimu lakini kwenye msawazisho ukiangalia mikoa mingine na hasa maeneo ya mjini bado takwimu zinaonesha kuna walimu wengi.

"Ni lazima Wizara zinazohusika kwa kuanza na Wizara ya TAMISEMI tufanye mapitio na kuleta walimu kwenye maeneo yenye uhitaji badala ya kuacha waendelee kuwepo kwenye maeneo ya Mji. Maeneo yote ya nchi hii yanahitaji huduma zinazofafana kama ni walimu basi tuweke msawazisho kote ili elimu itolewe kwa usawia na ulinganifu wa maeneo yote badala ya kutegemea kuwa na walimu kwenye maeneo ya Mjini na vijiji kukosa, hiyo inatuwekea tabaka wa upungufu wa wasomi kwenye maeneo ya vijijini.

"Sasa hivi shule za Serikali zipo kwenye kila eneo hivyo ni lazima tuzifanye kuwa bora na kimbilio la wananchi kupeleka watoto na kupata mafunzo kuanzia ngazi ya msngi mpaka sekondara, nitalisimamia na niwahakikishie Gairo na yenyewe itaongezewa walimu.

"Nimepata taarifa ndani ya Mkoa wa Morogoro kuna maeneo yanaziada ya walimu wengi tutapitia takwimu na tutaiagiza TAMISEMI kuratibu zoezi la kutoa walimu kwenye hayo maeneo kuja kwenye maeneo ambayo hayana walimu , ukiajiriwa na Serikali lazima ukubali kufanya kazi kwenye eneo lolote kwasababu lengo ni kutoa huduma na umewekwa ili ukawezeshe hilo ,

Kuhusu matokeo ya Kidato cha nne , Chongolo amesema yameshuka sana na hiyo inasababu kwani kama mwanzo walifanya vizuri kwanini mara ya pili wamefanya vibaya ,maana yake hapo lazima kunachangamoto."Kamisaa Wetu( Mkuu wa Mkoa) haya matokeo hayavutii wala hayafurahishi ni lazima tuweke mpango wa kupitia na kujua wapi tumejikwaaa mpaka tumeanza kushuka.

"Ni lazima tukae chini tupitie wapi tulipojukwaa turekebishe ili twende mbele tukipandisha kiwango cha ufaulu kwa watoto wetu,tusipowekeza kwa watoto kwenye elimu tutakuwepo na vijana ambao tija yake kwa nchi yao ni ndogo hivyo lazima tuwekeze kwa dhati kabisa kwenye elimu kwa vijana wetu, tuisimamie tukijua tija yake

"Na ninyi wazazi na ndugu wananchi ni lazima tujue tunawajibu wa kuwalea watoto wetu na kuwawezesha kupata elimu kwa kuwawekea miundombinu mizuri ya kupata elimu , Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejenga miungdombinu mingi sana ya elimu , madarasa yaliyojengwa mwaka 2021 na mwaka 2022 ni mengi sana.

"Kwa hiyo mabilioni ya fedha yameletwa ndani ya Mkoa wa Morogoro ikiwemo Wilaya ya Gairo na Mkuu wa Wilaya yenu amesema kwamba mmenufaika na madarasa hayo.Lazima tuweke nguvu kwenye kuwawezesha watoto wetu ,tusiwatoroshe kwa ajili ya kwenda kwenye mashamba kulima ,tusiwatoroshe kwenda kufuga mifugo ,tuhakikishe wanapata elimu."

Kuhusu mazingira, Chongolo amewapongeza Wilaya ya Gairo hasa jitihada zinazochukuliwa na Mkuu wa Wilaya huku akitoa rai kwa wananchi kupanda miti pembezoni mwa mito ili kuhakikisha mito haipanuki na kuleta madhara ya mafuriko na bahati nzuri ameona siku za kribuni jitihada za Wilaya katika kutunza mazingira ikiwa pamoja na kupanda miti.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo  akizungumza na Wanachama wa CCM Shina Namba 18 Kata ya Itaragwe, Kitongoji cha Matale, Halmshauri ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro.

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndg Daniel Chongolo, Akisukuma Chuma kinachoendesha mashine ya Kukamulia Juisi ya Miwa kwa ajili ya Utengenezaji wa Sukari Gulu inayozalishwa na Kikundi Cha Wanawake Cha Jitihada kilichopo kata ya Idiba Wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro,Akiwa katika Kikundi hicho Ameahidi kuwapatia Mashine Mpiya ya Kisasa ili kuongeza Utengenezaji wa Sukari Guru katika kikundi hicho

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndg Daniel Chongoloakisaini Kitabu Cha Wageni kwa Balozi wa Shina Namba 1 Katika Kijiji Cha Kidebya akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi ndg Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Organaizesheni Issa Haji Gavu Pamoja na Viongozi wa Chama Mkoani Morogoro.

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndg Daniel Chongolo akiwa pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi ndg Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe Ahmedi Shabibi wakati akikagua maendeleo ya Mradi wa Maji wa Serengeti Halmashauri ya Manispaa ya Gairo

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi ndg Sophia Mjema, Akitembea pamoja na Vijana Wa Hamasa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kumaliza mkutano Wa  Wanachama wa CCM Shina namba 18 Kata ya Itaragwe kitongoji cha Matale.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...