Na Mwandishi Wetu Michuzi TV -Kilombero

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa maagizo ya kuhakikisha mradi wa kituo cha kupozea umeme cha Kibaoni kilichopo Kilombero mkoani Morogoro kukamilishwa kwa haraka ili kuwaondolea wananchi aza ya kukatika umeme mara kwa mara.

Chongolo ametoa maagizo hayo leo baada ya kutembelea mradi wa kituo hicho ambao ujenzi wake haujakamilika kutokana na kutoanza kwa ujenzi wa Tower kubwa kwenye kituo hicho huku akielezwa mradi umefikia asilimia 84.5.

Akizungumza baada ya kupata taarifa ya kituo hicho, Chongolo amesema kwasababu ya umuhimu na malalamiko ya watu,umeme unakatika sana na imekuwa ni kero kubwa kwasababu unapokatika hauna taatifa mtu amewasha friji,amewasha TV,amewasha redio umeme unakatika ghafla maana yake vitu hivyo vinapata changamoto na muda wa kuanza kupima kujua ni nani kasababisha haupo.

"Sasa cha muhimu ili kuwasaidia wananchi kuondokana na hiyo adha ni kuhakikisha mkandarasi anamaliza hiyo kazi kwa wakati ,fedha ipo na kila kitu kipo na sisi viongozi lazima tuwe mbele kuhakikisha tunatatua changamoto ili mkandarasi anamaliza kazi kwa wakati.Kukamilika kwa kituo hiki itakuw suluhisho la kukatika kwa umeme kwa wananchi wa Malinyi,Ulanga na Kilombero.

"Kama wote watapata unafuu wa kukatika kwa umeme kupitia hapa ni lazima sisi tukae sawa sawa na tumeaambiwa kwamba material ya kutengeneza zile nguzo zinaletwa hivyo lazima zitengenezwe ziletwe lakini hata kitako cha Tower ambayo inasubiriwa angalau ujenzi wake ungeanza wakati vifaa vikisubiriwa.

"Mchanga ,sementi, kokoto ziko hapa basi angalau tuone hata ujenzi wa kitako cha Tower unaanza na vifaa vianze kufungwa wakati tunasubiri ujenzi wa hiyo tower hii angalau itatupa moyo,tukikaa na namna hii halafu tukifika hapa unatumbia pale itakuwa structure ya tower na tower yenyewe nacho kitako kinasubiri hii tunakuwa hatutendi haki ,sisi lazima tuwe mbele tuoneshe nia na dhamira ya kufanya mambo yaishe haraka,"amesema na kuongeza siku chache zijazo wananchi wataanza kuona kitako cha tower kinaanza kujengwa katika eneo hilo

Awali wakati akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu CCM , Meneja Usimamizi wa Miradi  REA Mhandisi Romanus Lwene  amesema kuna matatizo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na umeme umekuwa mdogo kwa hiyo ndio iliyosababisha kituo hiko kiweze kujengwa kitakapokamilika wananchi wa Wilaya za Kilombero na Ulanga.

"Umeme uliopo kwa sasa unatoka laini yenye uwezo wa kubeba megawati 8.3 kwa Wilaya zote mbili za Kilombero na Ulanga maana yake kama watu wanataka kutumia kwa uzalishaji na matumizi yakawa ,makubwa umeme unakatika kwani mwisho megawati 8.3. Kwa hiyo kwasababu hiyo Serikali ikafikiria kuweka kituo hiki hapa

Amefafanua kwamba mradi huo inatekelezwa katika mafungu mawili ,dungu la kwanza ni kuweka Substations ambayo inatekelezwa na mkandarasi wa Kampuni ya Spain kwa gharama ya Sh .bilioni 1.9 pamoja na Euro milioni 4.9 na Kwa zote hizo ni kama Sh. bilioni 13 na mradi wa kusambaza umeme ambao ulikuwa unatekelezwa na kampuni ya Burhan Engineering wenye unatumia jumla ya Sh.bilioni 6

"Huyu Burhan Engineering fungu la pili alikuwa anapeleka umeme kwenye vijiji Saba na vitongoji 8 jumla maeneo 15, alikuwa anajenga umeme urefu wa laini zenye urefu kilometa 78 Mv na LV kilometa 75 na kuweka transfoma 26 na alitakiwa aunge wateja 1858 na ameshaunga tayari wateja 1600, yeye alikamilisha Aprili mwaka jana na tower amefunga.

"Kwa hiyo tumebaki na kazi ya kituo Cha kupozea umeme ambacho anatakiwa akamilishe Machi mwaka huu , awali ilikuwa akamilishe Mei lakini kwasababu Kampuni ambayo imejenga hapa ni ya Ulaya na wenzetu walikuwa wamekumbwa na ugonjwa wa COVID-19 na material mengi tunanunua nchi za Ulaya na sasa kidogo kuna tatizo la Vita ya Ukraine kuagiza mzigo inakuwa tatizo

"Tulikaa nao na kuwaambia lazima mradi ufike mwisho kwa hiyo mradi unatakiwa kuisha

Machi 31 mwaka huu na kama kila kitu kingekuwepo wangeweza kumaliza lakini vifaa vimeshagizwa ila isipokuwa Tower ndio bado haijajengwa ambayo sasa iko kwenye utaratibu wa kuitengeneza."

Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwenye Ziara hiyo ameambatana na Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu kwa ajili ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho pamoja na kuzungumza na Makundi mbalimbali.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akitoa maagizo kwa  Meneja Usimamizi wa Miradi  REA Mhandisi Romanus Lwene ya kuhakikisha mradi wa kituo cha kupozea umeme cha Kibaoni kilichopo Kilombero mkoani Morogoro kukamilishwa kwa haraka ili kuwaondolea wananchi adha ya kukatika umeme mara kwa mara.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akimsikiliza  Meneja Usimamizi wa Miradi  REA Mhandisi Romanus Lwene alipokwenda kutembelea mradi wa kituo cha kupozea umeme cha Kibaoni kilichopo Ifakara,Kilombero mkoani Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...