Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe limepitisha Bilioni 30.6 rasimu ya mpango wa bajeti ya maendeleo ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 na kutoa mapendekezo kwa watendaji kwenda kuongeza nguvu ya ukusanyaji mapato.

Kauli hiyo imetolewa leo na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli kwenye kikao cha bajeti cha halmashauri hiyo kilichofanyika wilayani Njombe.

Amesema madiwani wanatakiwa kusimamia vizuri miradi inayoendelea kutekelezwa katika halmashauri hiyo na kutenga fedha asilimia 40 kumi kwa ajili ya mikopo ya vijana, wakina mama na watu wenye ulemavu na thelathini kwa miradi ya maendeleo.

"Ili tuweze kutekeleza vizuri bajeti ijayo tunahitaji kukamilisha miradi yote ambayo tumeipanga hasa kupitia mapato ya ndani" amesema Hongoli.

Amesema katika kutekeleza miradi ya kimkakati inatakiwa ushirikiano na usimamizi mkubwa wa makusanyo ya mapato na kupeleka fedha kwa wakati katika miradi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Sharifa Nabalang'anya amesema kupitia bajeti hiyo halmashauri inatarajia kutekeleza na kubuni miradi mbalimbali ya kimkakati ili kuongeza mapato ya halmashauri.

Amesema kabla ya kupitishwa kwa bajeti hiyo asilimia 70 ya mapato ya ndani yalikuwa yanategemea eneo moja pekee la misitu lakini sasa wanakwenda kuondokana na hali hiyo.

Amesema kutokana na mafunzo waliyoyapata baada ya kutembelea halmashauri za Chalinze na Dodoma yameleta matokeo makubwa na yameanza kuonekana.

"Kwasababu ni nadra sana kwa madiwani kukubali kupeleka zaidi ya milioni 600 kwenye miradi ya uwekezaji kwa mwaka mmoja wa fedha" amesema Nabalang'anya.

Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo akiwemo Neema Mbanga amesema shule ya secondari Lupembe inakabiliwa na changamoto ya bweni hivyo pamoja na jitihada za wananchi katika kuchangia ujenzi lakini wanahitaji nguvu kutoka serikalini.

"Bweni la sekondari Lupembe nguvu ya wananchi imetumika na maeneo yaliyobakia kama vyoo na rangi wananchi hawawezi " amesema Mbanga.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...