Na Lusajo Mwakabuku – WKS
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu la kuitaka nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 77 utakaojumuisha nchi wanachama wa kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Rais Samia ameridhia ombi hilo lililotolewa na Prof. Lumbu aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na Rais na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya Haki za Binadamu na Watu huku akiambatana na wadau wa asasi za kiraia za kutetea haki za binadamu za hapa nchini leo Tarehe 30/01/2023.

Awali kabla ya kuwasilisha ombi hilo, Prof. Lumbu alianza kwa kupongeza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza ambapo makundi mbalimbali yameonekana kupewa nafasi ya kujieleza yakiwemo makundi ya wanasiasa, Pia aliongelea suala la uhuru wa vyombo vya Habari ambao unaonekana kuimarika na jitihada mbalimbali zilizofanyika katika kukuza matumizi ya Lugha ya Kiswahili.

Baada ya pongezi hizo Prof. Lumbu aliwasilisha ombi hilo rasmi kwa Mhe. Rais huku akimuomba pia kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo ambapo Mhe. Rais aliahidi kutoa jibu baadae juu ya hilo.

Akiongelea suala la maendeleo ya haki za binadamu, Rais Samia alisema anaamini kuwa matatizo ya ndani yanaweza kumalizwa na sisi wenyewe na sio mtu wa nje na ndio maana alifikia hatua ya kukutana na vyama vya upinzani na kuangalia changamoto ni nini na baada ya majadiliano ikafikia hatua ya maridhiano yaliyopelekea pande zote kuwa kauli moja na hivyo kuondoa migongano.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu alipofika Ikule ya DSM leo 30/01/2023.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Damas Ndumbaro na viongozi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na asasi za kiraia za watetezi wa haki za binadamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...