-Ataka ujenzi Juni mwaka huu uanze, Serikali imeshatoa fedha...wananchi wanataka barabara

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Brabara ( TANROADS) Mkoa wa Morogoro kuhakikisha hadi ifikapo Juni mwaka huu ujenzi wa barabara ya kutoka
Ifikara kwenda Lupilo hadi Malinyi na nyingine inatoka pale Lupilo kwenda Mahenge.

Chongolo ameyazungumza hayo leo Februari 02, 2023 Wilayani Ulanga katika kikao cha
shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro,ambapo amesema baada ya kukagua ujenzi wa barabara inayotoka daraja la Kidatu kwenda Ifakara ambapo mkandarasi yuko kazini na Oktoba mwaka huu itakuwa imekamilika na tayari ameshazungumza na Meneja wa barabara Mkoa wa Morogoro.

"Sasa hivi Mkandarasi anaonekana yuko barabarani lakini tumekubaliana ikifika Oktoba suala la daraja la Kidato pamoja na hiyo barabara iwe historia. Wakati nakuja huku leo asubuhi nimezungumza na Rais Samia Samia Suluhu ameniuliza kuhusu barabara hiyo...

"Nikamwambia tumekubaliana na Meneja wa barabara iwe imekamilika Oktoba mwaka huu.Pia akaniambia alikuwa amewaagiza watangaze barabara ya kutoka daraja la Kilombero kwenda Lupilo huko Malinyi na kwenda Mahenge na tayari wameshatangaza tangu Oktoba ,2022 na kufungua zabuni.

"Ndugu wananchi mmemsikia Meneja wa Barabara Mkoa wa Morogoro kwamba Serikali ilishatoa fedha kujenga barabara kutoka Ifakara mpaka Lupilo na pale Lupilo inagawanyika kwenda Malinyi na nyingine inatoka pale Lupepo kwenda Mahenge barabara hii imeshatangazwa zabuni ambayo ilifunguliwa tangu Novemba ,2022 , sasa hivi timu ya watalaamu inafanya tathimini ili kumpata Mkandarasi wa kuijenga kwa kiwango cha lami.

Chongolo amefafanua imeshatangaza zabuni na wamekubaliana lazima mpaka Juni mkandarasi awe site na wananchi wanataka barabara sio maneno ya mchakato ,upembuzi yakinifu.Nani anajua?Watu wanataka barabara ianze kuchimbwa, ijengwe ndio watu wataamini tunachokisema.

"Sasa tumekubaliana mwezi wa Sita Mkandarasi awe Site aanze kujenga, wakati barabara inayotoka Kidatu kuja Ifakara inakamilika tunataka kuona lami sasa sio ya kuburuza buruza bali yenye hadhi. Mahenge ni Wilaya ya kihistoria, Mahenge ndio iliyoigawa Kilombero ,ndio imeigawa Malinyi sasa hauwezi kuwa mama unazaa watoto halafu wanapata raha wewe unapata shida.Mnazaa mtoto anafikishiwa barabara nyie wenyewe bado sasa umeitwa Makao Makuu ya nini ?

"Sasa tumekubaliana na hiyo barabara sio deni tena watekeleze kwasababu fedha ipo ikiifika Juni tunatarajia kuona vifusi lakini niseme ukweli barabara ujenzi wake sio sawa na kupanda mti ,ujenzi wake unautalaam mwingi ndio maana unaona kila hatua wanachimba udongo wanaenda kupima na ili iitwe barabara inatakiwa utalaamu.

" Watu wengi wanadhania mtu yoyote anaweza akajenga na hasa tunapozungumzia barabara hii kubwa , barabara ambayo imeanzia pale darajani ukienda mpaka Malinyi njiapanda pale ni kilometa 110 na kutoka pale Malinyi Center ni kilometa 10 na kwa ujumla barabara urefu wake ni kama kilometa 160 na ujenzi wa kilometa moja ni Sh.bilioni moja ,kwa hiyo tunazungumzia Sh bilioni 200 ambazo ni fedha nyingi

"Serikali imezitafuta imezitenga lazima ijiridhishe na mambo kadhaa la kwanza itafute mkandarasi mwenye hadhi na uwezo unaoendana na aina ya barabara tunayotaka kujenga. Kwa hiyo huwezi kuchukua mkandarasi yoyote na hatua za kufuata kupata mkandarasi huyo lazima utangaze na Sheria inataka ukitangaza huitangazi hapa ndani bali unatangaza duniani ili mwenye uwezo,"amesema.

Awali wakati anazungumza na wananchi Chongolo amewaomba waendelee kuiamini Serikali,waendeeeni kuiamini Chama Cha Mapinduzi ambacho Rais Samia yeye ndio Mwenyekiti wake kwani kimeidhamiria kutatua changamoto kwa kasi kubwa mpaka zote zikapokoma.

Aidha amesema mwaka 2020 walipewa dhamana ya kuongoza nchi na kazi ya kuongoza nchi haitaki uwe lele mama ni lazima uwe sawa sawa na wao( CCM)kwasababu wanadhamana hiyo wametoka ofisini kushuka chini kwa wananchi kuona nini kimefanyike na nini kilichoahidiwa na Kiko kwenye hatua gani ya utekelezaji.

Nae Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Sophia mjema amesema ni muhimu kwa Wana CCM kuuelezea Umma kuhusiana na Mafanikio ya Serikali kupitia Chama hicho, hasa katika Utekelekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, Uboresha Sekta ya Afya, Elimu, Umeme, Kilimo pamoja na miundo mbinu mbalimbali.

"Niwasihi Wana CCM kuwa kazi yenu kubwa ni kukisemea Chama cha Mapinduzi kutokana mafanikio yaliyopatikana, Kuyazungumzia mazuri yaliyofanywa na Serikali kupitia CCM chini ya Mwenyekiti wetu Dkt Samia Suluhu Hassan'" ameleeza Mjema.

Kwa Upande wake Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu amewasisitiza Wana CCM na Wananchi wa Ulanga kuwa na wajibu wa kulinda na kudumisha amani iliyopo, hatua ambayo itakuwa kichocheo cha kuendelea kujileletea maendeleo na kufungu zaidi milango kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo anaendelea na ziara yake ya Siku 9 mkoani Morogoro akiambatana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu.


Katibu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akisisitiza jambo Mbele ya Wajumbe wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla kwenye mkutano uliofanyika kwenye mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungumza mbele ya Wajumbe na wananchi kwenye mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro.Chongolo ameongozana Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu.
Katibu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba alipokuwa akieleza maendeleo ya ujenzi wa barabara mbalimbali ndani ya Wilaya ya Ulanga kwenye mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema akizungumza na Wajumbe pamoja na Wananchi kwenye mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema akiteta jambo na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Haji Gavu wakati wa mkutano wa Shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro
Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Salim Hasham akizungumza Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Danie Chongolo akiwasilisha mambo mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo kwa Wananchi kwenye mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro



Wajumbe wa mkutano wa shina namba 5,Ibwilonge,Mahenge mkoani Morogoro wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo amehuduria akiwa sambamba na viongozi wengine aliombatana nao kwenye ziara yake ya siku 9 mkoani Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...