Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge, ametolea ufafanuzi sakata la bomoabomoa ya nyumba ,katika kitongoji cha Matuga kata ya Kawawa na Zegereni wilayani Kibaha na kusema endapo kama hawajaridhika na maamuzi ya baraza la ardhi wilaya ,wafuate Utaratibu wa kisheria kukata rufaa ama wapate zuio la mahakama ya Mkoa kwani utekelezaji huo haujakurupushwa unatekelezwa kwa mujibu wa sheria.

Kunenge ameeleza Serikali ya mkoa wajibu wake ni kushughulika na yale ambayo wana wajibu nayo ili kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama utekelezaji unafanyika kwa mujibu wa sheria na sio kuingilia maamuzi ya mhimili wa baraza la ardhi ama mahakama.

Akitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo wakati alipoulizwa kama mkoa ni hatua gani wanaichukua , Kunenge alieleza Serikali ya mkoa inafahamu na kwamba nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba ina mihimili mitatu mahakama, Serikali na Bunge.

"Mihimili hii inafanya kazi bila kuingiliwa ingawaje mihimili hii inashirikiana ,inapotokea migogoro mbalimbali mfano upande huu wa ardhi, migogoro hii inaweza kutatuliwa kiutawala ,Lakini pia inaweza kutatuliwa kisheria kwa kwenda katika mahakama na kwa mujibu wa sheria zetu migogoro inaweza kutatuliwa katika mabaraza ya ardhi ya wilaya na mahakama "alifafanua Kunenge.

Kunenge alieleza, inapotokea Maamuzi yanafanyika aidha na baraza la ardhi na mahakama na ikatokea mtu hajaridhishwa na maamuzi hayo Utaratibu ,unatakiwa akate rufaa ama apate zuio katika ngazi ya juu zaidi ya ile iliyofanya Maamuzi.
"Na endapo itatokea dharura na mhusika akaona Kuna Maamuzi yanatakiwa kutekelezwa akate rufaa ama apate zuio la utekelezaji wa amri ile huku akiendelea na Utaratibu mwingine wa kupanda ngazi ya mahakama ya mkoa."

Awali Mkuu wa wilaya ya Kibaha Nikson John alipoulizwa juu ya mgogoro huo ambao inadaiwa mmiliki halali wa eneo hilo ni OMARI KADRI ,katika hukumu iliyotolewa katika kesi namba 176/2022 na kufunguliwa dhidi ya wadaiwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Zegereni na Baltazar Saimon alieleza, hiyo ni amri ya Mahakama,kama wapo walioguswa na hukumu wana haki ya kukata rufaa kwani Mahakama inahojiwa kwa mchakato wa kimahakama.

Nae Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Constantino Mwakamo alifika kutoa pole kwa wahanga na kusema walioguswa na bomoabomoa hiyo watafuataje Utaratibu wa zuio ama rufaa wakati katika kesi hawakuhusishwa Wala kutajwa.

"Kesi hiyo ilitambulika baina ya mmiliki KADRI dhidi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Zegereni pamoja na Bartazar Saimon Lakini cha kustaajabisha katika Maamuzi wameingizwa na maeneo mengine ya Matuga, Kawawa ambao hawakuhusika kwenye kesi."

"Kinachoshangaza ni hiki , huyo Kadri kwenye kesi yake hawakuwepo Wakazi wa Matuga Sasa imekuwaje waingizwe katika Maamuzi ya kubomolewa Tena bila kupewa notisi ya kubomolewa Wala kupewa taarifa ya sakata Zima"alifafanua Mwakamo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kijiji Cha Matuga ,Jofrey Kazinduki alieleza hadi sasa eneo la Matuga pekee wameshabomolewa nyumba takriban152 kati ya hizo nyumba za kisasa ni 131 na za vibanda vya kawaida 21.

Alieleza, kwasasa wahanga wanaishi kwa majamaa ,ndugu , wengine wamejihifadhi shuleni kusubiri hatma yao na kuongeza wanashindwa kwenda kuweka zuio kwakuwa hawajawahi kushtakiwa na kesi haikuwataja zaidi ya Zegereni hivyo kutokana na Serikali mkoa kuwapa ushauri watakwenda mahakama ya mkoa kutoa malalamiko yao.

Happy Festo mama wa watoto wanne mkazi wa kijiji cha Matuga ,alisema alikuwa akiishi hapo baada ya dada yake kumpatia eneo ili aishi na watoto kulingana na ugumu wa maisha , alibainisha kwa sasa yupo kwenye hali ya sintohamu kwani hana pa kuishi zaidi ya kujihifadhi kwenye banda.


Aliiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia ambao wana watoto na ambao hawana msaada wowote kwani hata Kama haiwezi kuingilia mhimili mwingine kisheria ,waangalie usalama wa raia na kuwa nao karibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...