Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


Timu ya taifa ya Senegal imeibuka kuwa Mabingwa wa Michuano ya Mataifa ya Afrika, kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN) baada ya ushindi wa jumla ya mikwaju ya ‘Penalti’ 5-4 dhidi ya waandaji wa Michuano hiyo, timu ya taifa ya Algeria.

Mchezo huo wa Fainali ulipigwa kwenye dimba la Nelson Mandela jijini Algers nchini humo, ulishuhudiwa na mashabiki lukuki katika dimba hilo, timu hizo zilienda sare ya 0-0 katika dakika 90’, huku Mwamuzi kutoka Gabon, Atcho Pierre Ghislain alilazimika kuongeza dakika 30’ na kufanya dakika hizo kuwa 120’ Milango ikiwa migumu (0-0).

Mwamuzi huyo kutoka Gabon, Pierre Ghislain aliamuru mikwaju ya ‘Penalti’ baada ya kuhitimishwa mchezo huo kwa Milango yote kuendelea kuwa migumu kwa dakika zote 120’. Katika mikwaju hiyo, Senegal walipata bahati ya kuondoka na ushindi huo wa mikwaju mitano dhidi ya mikwaju minne ya Algeria.

Katika tuzo zilizotolewa baada ya Michuano, Golikipa bora wa mashindano ni Pape Mamadou (Senegal), Mfungaji bora wa mashindano ni Aymen Mahious (Algeria), Mchezaji bora ni Houssam-Eddine Mrezigue (Algeria) na timu yenye nidhamu ni Mabingwa Senegal.

Michuano hiyo ikiwa kwenye makala ya saba hadi sasa, timu ya taifa kutoka ukanda wa Afrika Magharibi, ni Senegal pekee ndio waliotwaa ubingwa wa Michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009, Michuano hiyo ikifanyika nchini Ivory Coast.

Mataifa ambayo yametwaa ubingwa wa Michuano hiyo ya CHAN, ikiwa katika makala ya saba ni DR Congo, Tunisia, Libya, Morocco na Senegal ambao wameondoka na taji hilo mwaka wa 2022 katika mashindano yaliyofanyika mwaka huu wa 2023 nchini Algeria.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...