Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Kodi Ilala na Kariakoo kwa kushirikiana na Assad Associates wameendesha semina kuhusu mfumo wa kodi wa kielektroniki ulioboreshwa.

Akizungumza  wakati wa ufunguzi na wadau wa  
Semina hiyo iliyofanyika Februari 2,2023 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga, jijini Dar es salaam, Kaimu Kamishna wa kodi za ndani Bw. Michael Mhoja amesema, mfumo huu mpya wa kodi ulio boreshwa utaweza kutataua changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili walipakodi hasa wale wanaowasilisha ritani zao kwa njia ya mtandao. 

Aidha amewaomba wadau na watumiaji wa mfumo huo kuutumia kikamilifu ili kuokoa muda kwani wataweza kujihudumia kupitia mfumo huo ulioboreshwa.

 "Sasa kutakuwa hakuna haja tena ya kutembelea ofisi za TRA kwa mambo ambayo unaweza kuyafanya mwenyewe ukiwa unaendelea na shughuli zako kwa kupitia mfumo huu". 

Pia Bw. Michael Mhoja amewaomba wafanyabiashara na wanunuzi kutoa na kudai ristiri sahihi za EFD kwenye mauzo na manunuzi wanayofanya. "Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutoa risiti zenye ela pungunfu kulinganisha na bidhaa wanazouza sasa ukibainika utakumbana na adhabu"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo amewapongeza wadau hasa wafanyabiashara walioweza kuvumilia kipindi chote ambacho walipata changamoto za kimtandao wakati wa kuwasilisha ritani zao. 

"Najua kuna baadhi yenu mlipata changamoto kuwasilisha ritani hasa tarehe za mwisho za kuwasilisha ritani hizo lakini niwashukuru kwa uvumilivu wenu". Aidha Bw. Richard Kayombo amewataka wafanyabiashara na watumiajia wa mfumo huo ulioboreshwa wasisite kuwasiliana na TRA endapo watapata changamoto yoyote kwenye kutumia mfumo huo.

Kwa upande wao wafanyabiashara na watumiaji wa mfumo wa kodi wa kielektroniki wameipongeza TRA kwa kuweza kuboresha mfumo huo kwani utaondoa changamoto na kero walizokuwa wakizipata hapo hawali.



















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...