Na Mwaandishi Wetu Mtwara

MKURUNGEZI Mtendaji wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini Erica Yegella leo ameongoza kamati ya uhamasishaji wilayani humu kutembelea kata na vijiji katika Halmashauri hiyo kuhamasisha wananchi kushiri katika mapokezi ya mwenge wa Uhuru 2023 Aprili 3 mwaka huu.

Yegella pia ametembelea na kukagua miradi ambayo itapitiwa na Mwenge huo ikiwemo mradi wa Shamba la mikorosho, mradi wa maji na mradi wa bweni la watoto wa kike wenye mahitaji maalumu.

Harakati hizo zinafanyika ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kuzinduliwa Kwa Mbio za Mwenge huo Kitaifa katika mkoa wa Mtwara tarehe mosi Aprili mwaka huu.

Baada ya uzinduzi, Mwenge huo utakimbizwa katika Halmashauri ya Mtwara Vijijini Aprili tatu na nne.

Mratibu wa Mbio za Mwenge Halmashauri ya Mtwara Vijijini Nicholas Muya amesema jumla ya miradi mitano yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya hiyo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...