Na Mwandishi Wetu

DIWANI wa Kata ya Mzimuni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, Manfred Lyoto ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha nia kubwa ya kufikia malengo ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania.

Pongezi hizo zimetolewa na Lyoto wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi wake .

“Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiwataka viongozi kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kustawisha uchumi wa nchi na kuacha urasimu na unyanyasaji dhidi ya kundi hilo muhimu kwa ustawi wa uchumi wa nchi,”amesema Lyoto.

Lyoto ambaye amekuwa akitekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM, hivi karibuni amewahi pia kupongezwa na kamati tendaji ya CCM kata ya Mzimuni kwa kujitolea kuwalipa posho watumishi wa afya wanaojitolea katika Zahanati ya Mzimuni.

Diwani huyo amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan amechochea maendeleo mengi katika kukuza uchumi na kusema kuwa hali ya kiuchumi kwa sasa , kutokana na wawekezaji wengi ambao awali waliamua kuhamisha biashara zao katika mataifa mengine kwa sasa wanaonekana kurudi nchini kwa kasi na hivyo nchi kunufaika kiuchumi.

Diwani Kata ya Mzimuni wilayani Kinondoni, Dar es salaam Manfred Lyoto akifafanua jambo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...