Wananchi wakifurahi huduma  ya maji.

WAKATI Tanzania ikiungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Maji Duniani, kampuni ya kutengeneza maji na nishati ya Davis & Shirtliff  imetoa wito wa uwekezaji zaidi katika pampu za maji zinazotumia mionzi ya jua ili kusaidia nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.

Ukosefu wa maji katika nchi zilizopo katika jangwa la sahara umepelekea ukame katika baadhi ya nchi na kusababisha ukosefu wa chakula.

Akiongelea kuhusu maadhimisho ya siku ya Maji duniani, Mkurugenzi wa Davis & Shirtliff, Edward Davis amesema njia pekee ya kuepuka ukosefu wa maji ni kuwa na pampu za uhakika zinazotumia nishati ya jua ambapo ni za gharama nafuu na zinatunza mazingira.

Amesema ndio maana kampuni yake imewekeza katika teknolojia kuhakikisha watu wa majumbani na viwandani wanaweza kunununua vifaa vya kuwawezesha kupata maji kwa urahisi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo.

Amesema ana amini tatizo la ukosefu wa maji litaisha endapo jamii itatumia teknolojia hiyo inayopatikana kwa urahisi badala ya kutegemea mvua zisizo na uhakika.

"Usukumaji maji kwa kutumia nishati ya jua umethibitika kuwa endelevu na ufanisi  kiuendeshaji,"

" Pia unatumia gharama kidogo na ni mzuri katika utunzaji wa mazingira, hivyo kupunguza gharama za upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya kaya na viwandani ikiwa ni pamoja na kilimo," amesema  Davis .

Lengo la Siku ya Maji Duniani 2023 ni kuharakisha mabadiliko ili kutatua shida ya maji na kutunza usafi wa mazingira. 

Siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Machi, ili kuhamasisha watu duniani kote kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la maji na kuzingatia usafi wa mazingira. 

Siku hii imekuwa ikiadhimishwa na Umoja wa Mataifa toka mwaka 1993. 

Lengo kuu la maadhimisho ya Wiki ya Maji hapa nchini ni kuungana na Mataifa mengine Duniani katika kutathmini utekelezaji, mafanikio, changamoto na kuainisha mikakati yakuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira na kusimamia utunzaji wa rasilimali za maji nchini. 

Kaulimbiu ya Siku ya Maji Duniani 2023
ni: “Kuongeza Kasi ya Mabadiliko katika Sekta ya Maji kwa Maendeleo endelevu
ya Uchumi”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...