Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mhe. Jerry W. Slaa (Mbunge) imeona tija na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kupitia TANESCO katika uwekezaji wa mradi mkubwa wa kusafirisha umeme kutoka Nyakanazi Kagera hadi Kigoma mjini wa kilovoti 400 kwa lengo la kufikisha umeme wa Gridi ya Taifa ambao utakuwa ni umeme wa uhakika na wenye ubora zaidi.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara katika kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme mkubwa cha Nyakanazi, Kagera Mhe. Slaa (Mbunge) amesema,
"Kazi iliyofanyika hapa ni kubwa, tija ya uwekezaji imeonekana. Na sisi kazi yetu ni kuja kuona hizi pesa bilioni 654.29 ambazo nyingine zimetoka benki ya dunia, nyingine zimetoka African Development Bank, nyingine zimetoka Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, nyingine zimetoka Mfuko wa Maendeleo wa Ufaransa (AfD) lakini nyingine zimetoka Serikali ya Tanzania. 

Fedha hizi zina tija kwenye uwekezaji? Na tija maana yake nini? Maana yake kama Kigoma, Kasulu, Kibondo walikuwa wanatumia majenereta ambao uzalishaji wake ni wa gharama kubwa, basi umetoka ule uzalishaji wa gharama kubwa umeenda umeme wa gridi ambao matokeo yake TANESCO inapata faida badala ya hasara kwa kuzalisha umeme kwa gharama nafuu", alisema Mhe. Slaa.


Naye Mkurugenzi wa Bodi ya TANESCO Mha. Abdallah Hashim kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo amesema, "Sisi kama Bodi tunahakikisha kuwa miradi hii yote yenye uwekezaji mkubwa sana tunaisimamia vizuri kila hatua na pia tunaitembelea miradi hii kuona tija
(value for money)".

Mha. Didas Lyamuya Kaimu Mkurugenzi Miradi TANESCO akitoa maelezo ya mradi wa Kituo cha kupokea, kupoza na kusafurisha umeme cha Nyakanazi, Kagera kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) walipokitembelea kituo hicho siku ya Alhamisi, tarehe 23 Machi, 2023.

Mkurugenzi wa Bodi TANESCO, Mha. Abdallah Hashimu akiongea na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) walipokitembelea kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme mkubwa cha Nyakanazi, Kagera siku ya Alhamisi, tarehe 23 Machi, 2023.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...