Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imepokea na kupitisha makadirio ya matumizi na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake.

Aidha, Kamati hiyo imeishauri Serikali kuongeza uwigo wa bajeti kwa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara hususani katika utafiti wa viwanda, utafutaji wa masoko ya bidhaa za Tanzania na uendelezaji wa miradi ya kimkakati na kieleezo ili iweze kitekeleza majikumu yake na kuendana na maendeleo yanayofanyika katika Sekta zinazozalisha malighafi za viwandani.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Mwakiposya Kihenzile (Mb.) wakati Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ikiwasilisha Taarifa ya makadirio ya matumizi na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Nao Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuwezesha uendelezaji wa sekta hiyo inayofungamanisha sekta zote za uzalishaji kwa ufanisi ili kuongeza ajira, pato la Taifa na kuleta maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi nchini.

Akiwakilisha taarifa ya makadirio hayo, Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) ameomba kutengewa jumla ya shilingi 117,817,998,000 kwa mwaka 2023/2024 ambapo kati ya fedha hizo, shilingi 74,251,494,000 ni Matumizi ya kawaida na shilingi 43,566,504,000 kwa matumizi ya maendeleo.

Aidha Dkt. Kijaji ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara itatekeleza maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa ili kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na kitimiza azima ya Serikali ya Awamu ya Sita ya ujenzi wa uchumi shindani wa viwanda na utafutaji wa masoko ya ndani na nje ya mazao na bidhaa za Tanzania.

Awali Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah ameieleza Kamati hiyo kiwa Wizara imeweka malengo na mikakati mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 inayolenga kiendeleza sekta ya uwekezaji viwanda na biashara kwa kushirikiana na sekta fungamanishi ikiwemo kilimo, mifugo, uvuvi, nishati madini, uchukuzi na ujenzi



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. David Mwakiposya Kihenzile (Mb.)akiongoza wajumbe wa Kamati hiyo kupitia na kujadili Taarifa ya makadirio ya matumizi  na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24  kwa  Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Machi 22, 2023 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.


Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara  Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) akijumuisha,maoni na mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Machi 22, 2023 wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya makadirio ya matumizi  na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24  kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.




Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakitoa maoni na mapendekezo mbalimbali wakati Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ikiwasilisha Taarifa ya makadirio ya matumizi  na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24  kwa Kamati hiyo Machi 22, 2023 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.





Baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara wakijibu Hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo  wakati Wizara ikiwasilisha Taarifa ya makadirio ya matumizi  na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24  kwa Kamati hiyo Machi 22, 2023 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwasilisha Taarifa ya makadirio ya matumizi  na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24  kwa Kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...