Na Khadija Kalili
MKE wa wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere Mama Maria Nyerere jana usiku Machi 25, 2023 ametunukiwa zawadi ya Malkia wa Nguvu ya mwaka 2023 kwenye kilele kilichofanyika kwenye ukumbiwa Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Tuzo hiyo ya heshima imetolewa na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ambaye pia ni mtoto wa mama Maria Nyerere.

Tuzo hizo za Malkia wa Nguvu zimefanyika kwa mara ya saba sasa zimeandaliwa na Clouds Media Group na kudhaminiwa na CRDB Benki, Kilombero Sugar, Bwana Sukari, Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), DSTV na Classic Finnishers.

Wanawake wengine walio pata tuzo kwenye vipengele mbalimbali.

Tuzo ya Uongozi imekwenda kwa Kamishna Generali wa Jeshi la Uhamiaji Anna Makakala.

"Namshkuru mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini pamoja na viongozi wote wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kwa kumpa ushirikiano katika kazi zangu za kila siku za kukitumikia taifa" amesema Kamishna Makakala mara baada ya kupokea tuzo hiyo ya Uhamiaji, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanesco Somoe Ismail aliyepata Tuzo ya Funguo ya maisha kusababisha kwa kuwashika mkono Malkia wengine katika eneo lake la kazi.

Tuzo ya Ubunifu na uvumbuzi ilikwenda kwa Tasila Melita ambaye amebuni mashine ya kuteketeza taulo za kike wanazotunia wanapokuwa kwenye hedhi, Tuzo ya Ustawi wa Jamii imenyakuliwa na Dkt.Stella Rwezahura ambaye ni Daktari bingwa wa damu ambaye ndiye alisimamia upandikizwaji wa uloto kwa wagonjwa 11 wenye saratani ya damu nchini huku Tanzania ikiwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kutoa matibabu haya.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo yake Dkt.Rwezahura amesema kuwa jamii inapaswa kuondokana na imani potofu kuwa ugonjwa huu ni wa kurogwa hivyo mara wanapogundulika wanatakiwa kwenda hospitalini mara moja kwa sababu unatibika ni wa kurithi kama ilivyo selimundu na upo duniani kote.

"Naishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kunipa nafasi ya kusoma na kuwa Daktari bingwa wa damu kwani wakati naanza kusoma kulikua na madaktari bingwa wa damu wawili tu na walikua wakikaribia kustaafu japo awali nilipenda kuwa daktari wa wanawake hivyo nilikubali ushauri niliopewa na kwa sasa nawajibika kwa ajili ya taifa langu najivunia hili na nawashukuru wote pamoja na familia yangu." Amesema Dkt. Rwezahura.

Wengine waliopata tuzo ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Foundatin Tuli Ester Mwambapa aliyepata tuzo ya mhamasishaji bora wa mwaka .

Tuzo ya Malkia anayesabababisha ajira ilikwenda kwa mmiliki wa Kampuni ya Zara Tours ambaye ametoa ajira kati ya 300 hadi 600 katika ya utalii nchini washindi wote wamepewa tuzo pamoja na hundi ya Mil.3 kila mmoja zilizotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

Usiku huo wa Malkia wa Nguvu 2023 umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Sophia Mjema na wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia  Ackson akikamkabidhi tuzo Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...