WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri   wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani)  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akizindua Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' hafla iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

 

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals' iliyofanyika leo Machi 26,2023 jijini Dodoma.

Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amezindua tuzo kwa wahadhiri wa elimu ya juu ambao tafiti zao zitachapishwa katika majarida ya juu ambapo chapisho litakalokidhi vigezo na kushinda litapata Sh milioni 5o.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Machi 26,2023 Jijini Dodoma  wakati wa uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri kwa watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hafadhi ya juu Kimataifa 'High Impact Factor Journals'.

Prof Mkenda  amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na kuimarisha uwezo wa nchi katika kufanya tafiti na ubunifu unaolenga kuchagiza maendeleo ya uchumi wa viwanda na kuboresha maendeleo ya watanzania.

Amesema juhudi hizi zinajumuisha, pamoja na masuala mengine, kuongeza fedha na kujenga miundombinu ya kisasa ya utafiti na ubunifu sambamba na kuongeza idadi ya rasilimali watu yenye weledi stahiki na morali.

“Katika kuimarisha juhudi hizo na kuhakikisha kwamba nchi yetu inazalisha matokeo ya utafiti yanayoakisi na kujibu changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi na yenye hadhi ya kimataifa.

“Wizara imeanzisha Tuzo ya kila mwaka kwa watafiti kutoka Taasisi za Elimu ya Juu za Umma na Binafsi nchini wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hadhi ya kimataifa `High Impact Factor Journals`,”amesema Prof Mkenda.

Prof Mkenda amesema upatikanaji wa washindi wa tuzo hiyo  utazingatia utaratibu na vigezo vilivyoainishwa katika mwongozo wa Kitaifa ambao umezinduliwa  na kuanza kutumika rasmi kushindanisha machapisho yaliyochapishwa ndani ya kipindi cha kuanzia  Juni 1  2022 hadi Mei  31  mwaka huu.

“Tuzo hii itaanza kutolewa kwa machapisho katika fani za Sayansi Asilia na Hisabati na Tiba,”amesema 

Aidha,Mkenda  amesema tuzo hiyo  itajumuisha cheti na fedha taslimu Shilingi Milioni 50 kwa kila chapisho litakalokidhi vigezo na kushinda.

Vilevile, tuzo hiyo itatolewa kwa machapisho yote yanayokidhi vigezo kwa mwaka husika kwa kuzingatia uwezo wa kibajeti. Amesema kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni moja. Amesema wahadhiri watakaohusika na tuzo hiyo ni wale waliofanya utafiti kwenye maeneo ya sayansi asilia, hisabati na tiba na matokeo ya tafiti zao kuchapishwa katika majarida ya juu ya kimataifa.

Prof Mkenda amesema kwa kawaida matokeo ya mtafiti yatachapishwa katika majarida hayo kama dunia itayatambua na kuona kuwa mtafiti amesogeza uelewa wa binadamu katika maeneo ya sayansi na tiba.

Amesema majarida yenye hadhi ya kimataifa yatachanguliwa kwa kwa kuzingatia kigezo cha “Impact Factor”ambacho  kinachoakisi ubora wa machapisho katika Jarida husika.

“Mwombaji lazima awe Mtanzania kutoka katika Taasisi yoyote ya Elimu ya Juu iliyothibitishwa na mamlaka husika nchini mathalan TCU na NACTVET.

“Kila chapisho linalokidhi vigezo na kushinda litapokea Tuzo moja pekee inayojumuisha cheti na shilingi milioni 50; na ikiwa litakuwa limehusisha waandishi wa kitanzania zaidi ya mmoja, kiasi hicho cha fedha kitagawanywa kwa kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika Mwongozo wa Tuzo

“Mchakato wa kupata washindi utasimamiwa na Kamati ya Tuzo ambayo itateuliwa na Wizara kwa kuzingatia vigezo na uwiano ulioainishwa katika Mwongozo wa Tuzo,”amesema Prof Mkenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...