Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Pasaka kila mwaka Alex Msama amesema kuwa tamasha hilo mwaka huu litafanyika katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo kinondoni Jijini Dar es Salaam na kwamba hakutakuwa na kiingilio,litakuwa ni buree.

Msama ameyasema hayo leo Machi 19,2023 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo kinondoni Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa waimbaji mbalimbali kutoka Tanzania na nchi za Afrika Mashariki watatumbuiza.

"Maandalizi ya tamasha la Pasaka yanaendelea vizuri, hapo awali tamasha letu lilitakiwa lifanyike uwanja wa Taifa, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu tamasha hili halitafanyika tena Uwanja wa Taifa na badala yake litafanyika katika viwanja vya Leaders club, kwa hiyo tamasha lipo kama kawaida tarehe 9 mwezi April,2023 na mpaka sasa waimbaji wengi wamethibitsha kushiriki" amesema Msama.

Aidha amesema kuwa Tamasha hilo pia litakuwa la kumshukuru Mungu katika kusherehekea miaka miwili ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kwamba watatumia nafasi hiyo kumuombea ili aendelee kuiongoza nchi ya Tanzania kwa amani.

"Tamasha letu pia ni la kumshuru Mungu kwaajili ya uongozi wa mama yetu , Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani kwa mafanikio makubwa, miradi mingi imeendelea, kila kitu kinaenda vizuri, tunaishi kwa amani na utulivu hivyo ni lazima tumshukru Mungu kwa uongozi wa Rais wetu" ameongeza Msama.

Kwa upande wao baadhi ya waimbaji watakaoshiriki kwenye Tamasha hilo, Upendo Nkone na Mwakilishi wa kundi la Zabron Singers Emmanuel Zabron kwa nyakati tofauti wametoa mwito kwa wananchi hususani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye Tamasha hilo, huku wakiahidi kukonga nyoyo za wapenzi wa Muziki wa Injili na kutoa burudani safi.

Naye mratibu wa Tamasha la Pasaka Bw. Emmanuel Mabisa amesema kuwa mpaka sasa waimbaji wote walioalikwa kushiriki kwenye Tamasha hilo wamethibitisha ushiriki wao na kwamba maandalizi yote yanaenda vizuri.

"Hayawi hayawi sasa yamekuwa, lile tamasha lililokuwa likisubiriwa kwa miaka mingi la Pasaka sasa kufanyika katika viwanja vya Leaders Club bure bila kiingilio, hivyo wananchi wasisite kutoka na familia zao kuhudhuria kwenye tamamsha hilo" amesema Mabupa.



Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Pasaka kila mwaka Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Machi 19,2023 jijini Dar kuhusu kufanyika kwa tamasha la Pasaka katika katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo kinondoni Jijini Dar es Salaam na kwamba litakuwa ni buree,halina kiingilio,kusho ni Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Upendo Nkone.

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akieleza namna alivyojiandaa kuwatumbuiza wapenzi wa nyimbo za Injili katika tamasha hilo April 9,2023 katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar



Mmoja waimbaji mahiri mwakilishi wa kundi la Zabron Singers, Emmanuel Zabron akieleza namna walivyojiandaa kuwatumbuiza wapenzi wa nyimbo za Injili katika tamasha hilo la bure kabisa April 9,2023 katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar


Mratibu wa Tamasha la Pasaka Bw. Emmanuel Mabisa amesema kuwa mpaka sasa waimbaji wote walioalikwa kushiriki kwenye Tamasha hilo wamethibitisha ushiriki wao na kwamba maandalizi yote yanaenda vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...