Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye (Mb) amewataka maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati na kuacha utamaduni wa kusubiri mpaka taarifa za upotoshaji zitokee ndio watoe taarifa za kujitetea.

Waziri Nape ameyabainisha hayo Leo Machi 29, 2023 wakati akizungumza katika kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Tuulishe umma taarifa sahihi na kwa wakati, ukiona inafikia hatua unatakiwa kutoa taarifa ya kujitetea basi ujue kuna mahali unakosea”, Amezungumza Waziri Nape.

Ameongeza kuwa, “Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano ndio mmebeba taswira na mitazamo ya taasisi zenu, taswira na mitazamo inatengenezwa hivyo ni wajibu wenu kutengeneza mitazamo chanya ya taasisi mnazotumika”.

Amesisitiza kuwa, kada ya maafisa habari ina umuhimu wa kipekee na iwapo wakitimiza majukumu yao ipasavyo wataongeza thamani na umuhimu wao katika taasisi wanazofanya kazi.

“Nimepokea changamoto zenu za bajeti na vitendea kazi, sasa nitoe wito kwenu wa kuhakikisha mnatimiza wajibu wenu ili ninapoenda kupigania haki zenu na nyie muwe mmeonesha thamani ya uwepo wenu”, amezungumza Nape.

“Uafisa habari ni ajira, ni jukumu la kulinda taswira ya taasisi yako, na pia ni fursa ya kubadili maisha binafsi na Taifa kwa ujumla iwapo ukifanya vizuri katika eneo lako”, amezungumza Waziri huyo.

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari


Waziri wa Habari, Mawaailiano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akifurahai jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Ndg. Daniel Chongolo wakati wa Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam leo Machi 29,






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...