NA FARIDA MANGUBE, MICHUZI TV MOROGORO.


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na matumizi ya fedha katika ujenzi wa Mabweni wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mabweni hayo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya hiyo Japhet Hasunga amesema kamati imeridhishwa na thamani ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa mabweni hayo na kuipongeza VETA kwa kazi nzuri walioifanya.

Aidha Kamati hiyo imeutaka uongozi wa VETA kutengeneza na kuweka samani katika mabweni hayo ili yaanze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya PAC Mhandisi Isack Kamwelwe amesema yeye kama mataalam ameridhishwa na ujenzi wa maabweni hayo na kwamba amewataka wakandarasi wazawa wanaopewa zabuni wajenge majengo yenye kulingana na viwango vinavyokubalika .

Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe, Omary Kipanga ameihakikishia kamati kuwa Wizara itatekeleza maagizo yote yaliyotolewa kwa kuanza na utengenezaji wa samani za mabwani.

“Kama Wizara tunarudi kujipanga na kuhakikisha mpaka ifikapo mwezi Aprili tuweze kupata milioni 54 na kukamilisha samani zote zinazohitajika katika mabweni haya ili vijana wanapokuwa wanafungua Chuo katika muhula ujao waweze kutumia Mabweni.”amesema Niabu Waziri Kipanga.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amesema mabweni hayo yameghalimu zaidi ya sh.bilioni Moja na kwamba Wizara ipo tayari kuyatunza kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Awali akisoma taarifa ya maradi wa mabweni mbele ya kamati ya PAC Kaimu Mkurugenzi Mkuu VETA CPA Anthony Kasore amesema mradi huo wa mabweni mawili yana uwezo wa kuchukua wanafunzi 96 ( walimu tarajili) ulioanza Agosti 2018 na ulipangwa kughalimu zaidi ya bilioni moja zitokanazo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa Serikali ya Tanzania.

Aidha mpaka sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na kwamba bado wanasubiri samani ili mabweni yaanze kutumika huku zaidi ya mafundi 97, mama lishe pamoja na watoa huduma mbalimbali walipata ajira katika mradi huo.

Amesema samani zinazohitajika katika mabweni hayo zinakadiliwa kuwa zaidi ya sh.Milioni 54 ambapo VETA imeomba fedha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...