Serengeti Breweries Limited (SBL) kupitia kampeni ya bia yake ya Pilsner lager iliyopewa jina la ‘ Kapu la wana’ imekabdihi zawadi ya pikipiki na zawadi nyingine kwa washindi saba katika droo yake ya tatu ya kampeni hiyo iliofanyika mapema wiki iliyopita na kubaini washindi kutoka Karagwe, Tanga na Mbeya

Kutoka droo ya tatu ya kampeni, washindi watatu waliondoka na simu za mkononi, washindi wengine watatu walipata seti za televisheni na mshindi mmoja alizawadiwa pikipiki. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwa wakati mmoja katika kanda ya Ziwa, Kaskazini na Kusini ambako kampeni ya ‘Kapu la Wana’ inahusika

Akizungumza katika hafla ya ukabidhiji mkoani Mbeya, mshindi wa pikipiki hiyo, George Minja alisema anafuraha kuibuka mshindi wa pikipiki hiyo kutokana na kampeni hiyo na kuongeza kuwa kampeni hiyo imekuwa msaada kwani inasaidia kuinua uchumi wa watumiaji wanapokuwa wakitunukiwa zawadi kama vile pikipiki ambazo wanaweza kuzitumia kujiongezea kipato, "kampeni hii imeonekana kuwa ya thamani kwetu watumiaji kwa sababu tunazawadiwa zawadi ambazo kwa namna moja au nyingine zinaendeleza maisha yetu na hii inadhihirisha ni kwa kiasi gani Pilsner Lager inatujali watumiaji.”

Kwa upande wake, Meneja wa SBL Kanda ya Kusini, George Rweyemamu aliwapongeza washindi hao, akisema dhumuni la kampeni ya ‘Kapu la Wana’ ni kuwajengea uwezo wateja wanaofanya kazi kwa bidii kwa kuwazawadia zawadi mbalimbali baada ya kushiriki kampeni hiyo, “tunathamini waheshimiwa wateja wetu. na, hii ni njia yetu ya kuwatuza kwa kupenda na kuunga mkono chapa yetu, hii ni mara ya tatu tunaendesha kampeni hii na kupitia kampeni hii tunataka kuwapa wateja wetu fursa ya kuinua maisha yao kwa njia moja au nyingine, kwa mfano mshindi wa pikipiki anaweza kuamua kuitumia ili kusaidia kuongeza mapato yake na kwa upande mwingine, washindi wa televisheni na simu mahiri zawadi zao zitaendeleza ustawi wao wa kijamii.”

Alitoa wito kwa watumiaji katika kanda za Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea kushiriki katika kampeni na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo ya muda wa wiki 8 ambayo ilizinduliwa tarehe 2 Februari. Zawadi hizo ni pamoja na runinga mahiri, simu mahiri, pikipiki na zawadi kubwa ya gari ambalo ni jipya kabisa.

Akielezea jinsi ya kushiriki Rweyemamu alisema, “baada ya kununua bia ya Pilsner, kwaruza ili kupata kadi ya zawadi. Ikiwa zawadi ni nambari ya msimbo itume kwenye namba 15320 k.m. andika kapu 4321 Iringa. (Ruka nafasi kati ya maneno) kisha SMS itatumwa kuthibitisha ushiriki na kupata nafasi ya kushinda."

SBL imewekeza jumla ya Tzsh 36 milioni katika kampeni ya kuwapata washindi 22 hadi mwisho wa kampeni. Katika droo ijayo ya nne na ya mwisho ya kampeni, zawadi kuu ya gari jipya itatolewa kwa mshindi wa bahati.



Meneja mauzo wa kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL) Kanda ya ziwa Magharibi  John Changae(kushoto) akimkabidhi zawadi ya TV mkazi wa Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera Frank Kichele wakati wa hafla ya utoaji zawadi za promosheni ya Kapu la Wana iliyofanyika Kayanga mkoani Kagera.

Meneja mauzo wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kanda ya kaskazini, Abel Mushi (kulia) akimkabidhi televisheni Frank Yohana (kushoto) ambae ni mmoja wa washindi wa promosheni ya bia ya Pilsner ijulikanayo kama Kapu la Wana. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...