Catholic Relief Services
(CRS) inajivunia kutangaza mwaka wake wa 60 wa kuwepo nchini Tanzania.
Ili kuadhimisha hatua hii muhimu, CRS inaandaa hafla mnamo Machi 28
kuwakaribisha viongozi wa serikali ya Tanzania, viongozi wa makanisa,
mashirika washirika, wafadhili, na wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa
CRS nchini Tanzania. Sean Callahan, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa
Catholic Relief Services, atajumuika kwenye hafla hii itakayofanyika Dar
es Salaam-Tanzania.
Akizungumzia tukio hilo, Callahan alisema
“wakati CRS duniani inatimiza miaka 80, ni heshima kubwa kuwapo
Tanzania kwa miaka 60, tukifanya kazi bega kwa bega na Kanisa Katoliki,
washirika wetu wa maendeleo na jumuiya tunazohudumia, na kazi hii
inaendelea kuwa jukumu kubwa kwetu kutokana na uaminifu tuliopewa."
CRS
imekuwa ikihudumia jumuiya za Kitanzania tangu 1962. Wakati ambapo
mahitaji ya kibinadamu yamefikia kiwango cha juu zaidi duniani,
tunaendelea kuunga mkono mabadiliko yanayochochewa na jamii kwa kiwango
kikubwa nchini kwa kufanya kazi bega kwa bega na viongozi wa dini
mbalimbali, washirika wa kitaifa na jamii mbalimbali katika njia yao ya
ustawi na ustahimilivu dhidi ya athari mbaya za changamoto kuu za leo,
ikiwa ni pamoja na masuala ya jinsia, upatikanaji wa masoko na fedha
kwa vijana, uhaba wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa.
Maadhimisho
ya miaka 60 ya CRS Tanzania yataanza Machi 28 kwa Misa ya Shukrani
katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay saa 8:00 Mchana,
baada ya misa, jumuiko la pamoja limeandaliwa katika Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam na kutakuwa na shughuli na maonyesho mbalimbali,
ikiwa ni pamoja na ukuta wa kumbukumbu unaoonyesha mafanikio makubwa ya
CRS kwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania, maonyesho ya programu za
sasa na zilizopita na hotuba kutoka kwa Rais wa CRS, Meneja CRS
Tanzania, kiongozi wa kanisa, na kiongozi wa serikali pamoja na shuhuda
kutoka kwa wafanyakazi na washirika, na uwasilishwaji wa ushairi wa
kisasa. Katika kuunga mkono dhamira ya Wizara ya Afya ya Tanzania ya
kuhakikisha afya na ustawi wa raia wote wa Tanzania katika mapambano
dhidi ya COVID-19, CRS itawezesha banda la chanjo ya COVID-19 katika
hafla hiyo.
Catholic Relief Services (CRS) imekuwa ikifanya kazi
na watu wanaoishi katika mazingira magumu zaidi katika jamii za
vijijini nchini Tanzania tangu mwaka 1962. Leo, programu ya nchi hii
inasaidia miradi ya afya, lishe na maendeleo ya utotoni, ushirikishwaji
wa kijinsia, uwezeshaji vijana na ujasiriamali, mabadiliko ya
tabianchi, pamoja na maji, na usafi wa mazingira(WASH).
Kwa habari zaidi, tembelea https://www.crs.org/our-work-overseas/where-we work/tanzania Catholic Relief Services (CRS) ni wakala rasmi wa kimataifa wa kibinadamu wa jumuiya ya Kikatoliki nchini Marekani. Shirika hili linapunguza umasikini na kutoa msaada kwa watu wanaohitaji msaada katika zaidi ya nchi 100, bila kujali rangi, dini au utaifa.
Kazi
ya misaada na maendeleo ya CRS inakamilishwa kupitia programu za
kukabiliana na dharura, VVU, afya, kilimo, elimu, fedha na kujenga
amani. Kwa habari zaidi, tembelea www.crs.org
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...