MTAYARISHAJI wa Kazi za filamu nchini, Chuchu Hans amesema tamthilia yake mpya ‘Jeraha’ ni maisha halisi ambayo yapo katika Jamii.

Chuchu Hans ambae kwa mwaka 2023 ameuanza vizuri kwa kuitambulisha tamthilia yake mpya "Jeraha'' amesema kazi hiyo imeshirikisha wasanii wakongwe na chipukizi lengo ni kutoa kitu chenye weledi kwa jamii.

Chuchu Hansa ameongeza kuwa tamthilia hiyo itaanza kuonyeshwa Machi 27 mwaka huu, katika kingamuzi cha Azam.

“Ndani ya tamthilia ya Jeraha kuna wasanii wakongwe watano ambao ni mimi mwenyewe, Vicent Kigosi ‘Ray’, Single Mtambalike ‘Richie’, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ na Mariamu Ismail."

Aidha amewataka watanzania watarajie kuona kitu cha pekee na kujifunza kupitia tamthilia hiyo iliyosheheni wakali mbalimbali hususani vipya vya zamani na vipya.

Kwa upande wake Single Mtambalike maarufu kama "Rich rich'' ambae ni miongoni mwa wasanii walioshiriki katika tamthilia hiyo.

Aidha, amesema Wasanii wanapaswa kusikiliza ushauri kwa waliowatangulia, pia kuongeza ubunifu wao kwa sababu mtarishaji wa tamthilia anaangalia mtu mwenye vionjo vingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...