Na John Walter-Manyara

Kwa mwaka wa fedha 2023-2024 TANROADS mkoa wa Manyara inatarajia kutumia shilingi Bilioni Bilioni 11.529.

Kazi wanazotarajia kuzifanya kwa mwaka ujao wa fedha ni pamoja na kuendelea kuupanua mlima Dabil katika barabara ya Dareda-Dongobesh, kuendelea kuongeza tabaka la lami sehemu zilizochakaa bara bara kuu ya Babati-Singida, Babati-Arusha na Babati-Dodoma, kujenga madaraja mawili katika bara bara ya mbuyu wa Mjerumani na daraja moja katika bara bara ya Dongo-Sunya-Kijungu maeneo ya Magomeni.

Akiwasilisha makadirio hayo katika baraza la Ushauri la mkoa (RCC) iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa, Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Manyara Mhandishi Dutu Masele, ameliambia baraza hilo kuwa wanatarajia kuendelea kuweka taa za barabarani katika miji ya Babati,Mererani , Kibaya, Endasak, Orkesmet, Katesh na kuendelea kuzifanyia matengenezo bara bara zote za mkoa kwa kuchonga na kuweka tabaka la changarawe.

Aidha wataweka mzunguko (ROUNDBOUT) katika makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Mbulu kwenye barabara ya kuelekea Mbulu mjini, Hydom na Dongobesh mjini.

Kuhamisha bara bara yenye urefu wa Mita 700 ili kuepusha kuvunja nyumba za makazi ya watu Orkesmet mjini.

Pia TANROADS mkoa wa Manyara imeomba fedha shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kazi za maendeleo ambapo zitatumika kuendelea kujenga kwa kiwango cha zege mlima Magara, na sehemu korofi katika bara bara ya Babati-Kiru sehemu ya mlima Kuta pamoja na kuendelea kuzifanyia marekebisho kwa kiwango cha Changarawe bara bara za mkoa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...