Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina yake na Marekani na inawakaribisha wawekezaji kutoka nchini humo kuja kuwekeza na kushirikiana na watanzania katika ufanyaji biashara katika sekta mbalimbali nchini.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na
kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji
baina ya nchi hizo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle
Machi 27, 2023 katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam.
Aidha,
Waziri Kijaji ameiomba Marekani kuongeza muda wa Mkataba wa Mpango wa
Ukuzaji fursa za Kiuchumi Afrika (AGOA) uliotiwa saini mwaka 2000 na
awamu inayotarajiwa kuisha ni kati ya 2015 na 2025.
Akifafanua
zaidi, Dkt. Kijaji amesema Mpango huo wa AGOA unalenga kutoa fursa ya
upendeleo kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kupeleka bidhaa
zaidi ya 6,500 bila kulipa ushuru wa forodha nchini Marekani
Dkt. Kijaji pia ameainisha kuwa Tanzania ni moja ya nchi inayonufaika na
fursa ya Mpango wa AGOA ambapo Sekta ya Nguo na Mavazi inachangia mauzo
kwa asilimia 95. Kutoka katika Viwanda vikubwa vya Mazava Fabrics and
Production E.A L, na Tanzania Tooku Garments Co., Ltd . Bidhaa zingine
zinazochangia asilimia 5 ni bidhaa za Mikono, Uchakataji bidhaa za
kilimo (Agro-processing) na Ngozi.
Naye Balozi wa Marekani nchini
Tanzania Mhe. Michael Battle amesema Marekani itaimarisha uhusiano wa
kibiashara na uwekezaji na Tanzania hususani katika sekta mbalimbali
ikiwemo viwanda na kufanya biashara na benki za kitanzania ili
kirahisisha upatikanaji wa mitaji kwa wafanyabiashara wa Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...