Na Muhidin Amri,Songea.

WAKALA wa Barabara za vijijini na mijini Tarura wilaya ya Songea,katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita imepokea jumla ya shilingi bilioni 19,190,960,200.2 kwa ajili ya kujenga,kukarabati na kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara.

Meneja wa Tarura wilaya ya Songea Mhandisi Bakari John alisema, kati ya fedha hizo shilingi bilioni 10,437,504,253.41 sawa na asilimia 254 zimetolewa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na shilingi bilioni 8,753,455,946.79 sawa na asilimia 196 ni za mwaka wa fedha 2022/2023.

Bakari alisema,ongezeko la fedha hizo ni kutoka serikali kuu kutokana na tozo ya shilingi 100 kwa kila lita moja ya mafuta(dizeli na petrol),fedha za mfuko wa barabara na mfuko wa jimbo.

Amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi wake na kumshukuru kwa kuweza kuongeza fedha kwenye bajeti ya Tarura wilaya ya Songea kwa asilimia 196 kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Alisema,fedha hizo zimesaidia sana kuchochea shughuli za uchumi na kurahisisha usafiri na usafirishaji na kuongeza uboreshwaji wa mtandao wa barabara za vijijini na mijini hasa katika wilaya ya Songea.

Alisema,ongezeko hilo la fedha imewezesha hali ya barabara kuimarika na kuboreshwa kwa kiwango cha lami,changarawe,udongo,ujenzi wa vivuko na madaraja ili ziweze kupitika kipindi chote cha mwaka.

Kwa mujibu wa meneja huyo wa TARURA ni kwamba,kabla Rais Dkt Samia Hassan kuingia madarakani bajeti ya Tarura wilaya ya Songea ilikuwa wastani wa shilingi bilioni 2,952,263,000.00 tu kwa mwaka.

Bakari alisema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Dkt Samia,Tarura wilaya ya Songea imepata mafanikio makubwa ikiwemo kuongezeka kwa barabara za lami kutoka kilomita 51.47 hadi kilomita 58.57.

Aidha alisema,barabara za changarawe zimeongezeka kutoka kilomita 345.70 hadi kilomita 457.17,barabara za udongo zimepungua kutoka kilomita 1,803.416 hadi kilomita 1,684.846 na idadi ya madaraja yaliyojengwa imeongezeka kutoka 125 hadi 150 na taa za barabarani kutoka 340 hadi 383.

Alisema,Tarura inaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati kwa kufungua barabara ili kufika kusikofikika,kuboresha barabara zilizopo,kusaidia maeneo yote kufika kwa wakati,kuunganisha huduma za usafiri wa barabara ndani ya wilaya,kupunguza gharama za uendeshaji wa vyombo vya moto,muda wa kusafiri na kufanikisha malengo na maono ya wakala.

Moses Nyilenda mkazi wa Songea,ameipongeza serikai ya awamu ya sita kwa kuendelea kufanya maboresho makubwa ya miundombonu ya barabara za mitaa katika wilaya ya Songea na mkoa wa Ruvuma.

Alisema maboresho hayo,yamesaidia barabara nyingi za mitaa katika manispaa ya Songea na maeneo ya vijijini kupitika kwa urahisi na kupanda thamani ya ardhi na amewaomba wananchi wenzake kutunza barabara hizo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kurahisisha shughuli mablimbali za kiuchumi.

 miongoni mwa Barabara za lami iliyojengwa na wakala wa Barabara za vijijini na mijini(TARURA)wilaya ya Songea.

Meneja wa Tarura wilaya ya Songea Mhandisi Bakari John kulia,akielekeza jambo kwa mhandisi Davis Mbawala kutoka Ofisi ya meneja wa Tarura wilayani humo,walipotembea ujenzi wa barabara ya Tunduru-Jct-Seedfarm inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...